Kuelekea Uchaguzi Serikali za Mitaa - Siku ya Uteuzi
Wagombea watawasilisha fomu za uteuzi kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kabla ya saa kumi kamili jioni baada ya hapo fomu hazitapokelewa ili kuruhusu kufanyika kwa uteuzi wa wagombea kutokana na fomu zilizowasilishwa."
• Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atafanya uteuzi wa wagombea wa nafasi za Uenyekiti, Ujumbe wa halmashauri ya Kijiji katika siku zisizopungua ishirini kabla ya tarehe ya Uchaguzi.
• Uteuzi utafanyika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na dakika kumi na tano jioni ya siku ya uteuzi.
• Baada ya uteuzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atabandika majina ya wagombea wenye sifa na wasio na sifa za kugombea mahali pa matangazo ya Uchaguzi.
• lkiwa hakuna mwombaji aliyejitokeza au kama waombaji wote waliojitokeza hawana sifa zinazostahili, utaratibu wote wa uteuzi utaanza upya.
• Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wengine wa Halmashauri ya Kijiji watatakiwa kujiuzulu nyadhifa zao siku tatu (3) kabla ya siku ya kuchukua fomu za kugombea Uongozi.
No comments:
Post a Comment