Katika kuhakikisha wananchi wa pembezoni mwa mji wanapata maji safi na salama,
Mamlaka ya Majisafi na majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA)
imedhamiria kuwapelekea maji wananchi wa Mkuranga ifikapo Desemba mwaka
huu.
DAWASA kwa kutumia fedha za ndani takribani bilion 5.6 wameanza
mchakato wa kupeleka mabomba na kuyalaza kwa urefu wa Km 15 kuanzia
kwenye mradi huo na kuepelekwa maeneo ya karibu ya Mkuranga..
Akielezea mikakati hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi
Cyprian Luhemeja amesema kuwa mkandarasi ataingia kazini mwezi Mei mwaka
huu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundo mbinu itakayowezesha kusambaza
maji kwa wananchi wa Mkuranga na maeneo ya karibu.
"Mkandarasi ataingia kazini Mwezi Mei mwaka huu, na kuanzia kesho
April 12 tutaanza kazi ya ulazaji wa mabomba yatakayokuwa na urefu kwa
Km 15,"amesema Luhemeja.
Luhemeja
amesema, mpaka sasa wananchi 2500 ndio wanaopata maji kati ya wananchi
25,500 na wamechimba kisima chenye urefu wa Mita 600 na kutajengwa tenki
litakalokuwa na uwezo wa lkuhifadhi maji Lita Milion 1.5 kwa siku.
Amesema, hii ni mikakati ya kufungua maeneo ya pembezoni na mradi huu
ukikamilika wananchi wa Mkuranga, Vikindu hadi Mbagala watanufaika kwa
kupata maji safi na salama.
Mhandisi Luhemeja amewaomba wananchi kuvumilia mpaka Disemba wataanza
kupata maji safi na salama ambapo yataondoa kero ya miaka mingi ya
kutokuwa na huduma hiyo.
Ziara
ya Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA inaendelea lwenye miradi tofauti
ambapo ipo kwenye hatua mbalimbali za umaliziaji na mingine ikiwa hatua
za awali kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata maji ya uhakika
hususani pembezoni mwa mji ambapo hakukuwa na mtandao wa maji wa DAWASA.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja
akisikiliza maelezo ya mradi wa Kisima cha Mkuranga, Pwani kutoka kwa
Msimamizi wa Mradi Mhandisi John Kirecha (wa pili toka kulia) wakati wa
ziara ya kutembelea kujionea maendeleo ya mradi huo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akionja maji ya kisima yatakayosambaziwa wakazi wa Mkuranga, Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa pili
toka kushoto) akiendelea kukagua mradi wa kisima kilichopo Mkuranga,
Pwani.
Picha na Cathbert
Kajuna - Kajunason/MMG.
No comments:
Post a Comment