SGR

Katiba

SGR

Friday, April 12, 2019

BALOZI SEIF AKUTANA NA PROF.KABUDI ZANZIBAR

652
 Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipofika kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
673
 Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi wa Pili kutoka Kushoto akielezea msimamo wa Wizara yake katika kuzitangaza fursa za Uwekezaji zilizopo Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Muombwa.
685
 Profesa Palamagamba Kabudi(katikati) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
688
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa kwanza kulia akimpongeza Profesa Palamagamba Kabudi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
693
Balozi Seif kulia na Profesa Palamagamba Kabudi wakibadilishana mawazo mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Vuga Mjini Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kuwa na Taifa linaloendelea kudumu muda wote kutokana na misingi imara iliyowekwa na Waasisi wa Taifa hilo.

Alisema yapo Makabila mengi katika Mikoa na Wilaya mbali mbali Nchini Tanzania lakini muungano wa sauti moja inayozungumnzwa na Wananchi wake Bara na Zanzibar imekuwa mfano kwa Mataifa mengine Duniani.

Profesa Palamagamba Kabudi alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar alipofika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.

Alisema yapo Mataifa mengi Duniani yaliyowahi kuunganisha Nchi zao akaitolea Mfano iliyokuwa Yugoslavia na sasa imesambaratika Senegal na Gambia kwa Afrika lakini zimeshindwa kuendeleza Miungano hiyo.

Waziri Palamagamba alisema wakati Serikali zote mbili Nchini Tanzania zinaendelea kuheshimu kwa kuweka Kumbukumbu za Waasisi hao Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Vizazi vya sasa vinapaswa kujifunza tabia ya Viongozi hao walioacha msingi imara wa Umoja ndani ya Ardhi ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment