Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo kwenye Jimbo la Arumeru Mashariki na Kata
Sita (6) za Tanzania Bara utakaofanyika Tarehe 19 Mei mwaka huu wakila
kiapo wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Jijini Dodoma leo (Ijumaa Tarehe 12.04.2019).
Amesema
chaguzi hizo ndogo zitajumuisha wapiga kura 211,741 waliojiandikisha
Katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika vituo 567 vya kupigia
kura.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bi. Givenes Aswile aliwakumbusha washiriki hao
wa mafunzo kuwa wanapaswa kuhakikisha kwamba chaguzi hizo zinafanyika
bila kuwa na dosari ili kupunguza malalamiko na mashauri mahakamani.
Kaimu
Mkurugenzi aliwakumbusha pia Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi hao
kuwa wanatakiwa kuwepo maeneo ya kazi muda wote katika kipindi cha kutoa
fomu za uteuzi, siku ya uteuzi, wakati wa kampeni, siku ya kupiga
kura, kuhesabu na kujumlisha kura hadi kutangaza matokeo ya Uchaguzi.
Bi.
Aswile aliwaambia kuwa wajiepushe na migogoro ya Vyama vya siasa kwa
kutotoa fomu za uteuzi kwa wagombea wawili wa Chama kimoja cha Siasa.
Kila Chama kinatakiwa kumdhamini Mgombea mmoja tu.
Wakati
wa Kampeni, Kaimu Mkurugenzi aliwakumbusha kwamba wanatakiwa kuunda
Kamati za Maadili Ngazi ya Jimbo kwa Ubunge na Kamati ya Maadili Ngazi
ya Kata kwa Udiwani ili kushughulikia kwa haraka malalamiko kama
yatakuwepo.
Kata zenye uchaguzi ni pamoja na Uwanja wa Ndege iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi, Kitobo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, Kyela iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, Mikocheni iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam, Mvuleni iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi na Manda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
|
No comments:
Post a Comment