Halmshauri
ya jiji la Dodoma limetumia kiasi cha Sh milioni 345 kutoka kwenye
mapato yake ya ndani kwa ajili ya kununua vitendea kazi ambavyo ni
magari matatu ili kuimarisha Kitengo cha udhibiti wa ujenzi holela chini
ya Idara ya Ardhi, Mipango miji na Rasimali.
![]() |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dodoma Godwin Kunambi akiongea katika hafla ya kukabidhi magari matatu yaliyonunuliwa na Halmashauri hiyo. |
Akikabidhi magari hayo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Binilith Mahenge amelipongeza jiji hilo kwa kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuhakikisha wanatekeleza Mpango kabambe wa jiji hilo uliozinduliwa hivi karibuni.
Amesema
mpango huo ulipangwa na kupitishwa na baraza la madiwani, na Mkurugenzi
wa jiji na Menejimenti yake wameteleza kwa haraka ni hatua kubwa.
"Waziri
Mkuu aliagiza kusimamia utekelezaji wa mpango kabambe wa jiji hili na
muda mfupi baada ya kutolewa agizo hilo nyinyi mmetekeleza mara moja kwa
kununua vitendea kazi ambavyo ilikuwa ni moja ya maelekezo, nawapongeza
kwa kutumia kiasi hicho cha fedha kutoka mapato yenu ya
ndani,"alisema Dkt Mahenge.
![]() |
Moja ya gari lililonunuliwa na Halmashauri ya jiji la Dodoma kwa mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuimarisha kitengo cha udhibiti wa ujenzi holela. |
Ameongeza
kusema“Kwa kuwa na vitendea kazi hivi hatutegemei kuona tena ujenzi
holela Dodoma,hatutegemei kuona X maana hiyo alama inaonyesha kuwa huyo
mtu hakutembelewa kabla,hatutegemei kabisa kabisa kuona ujenzi kwenye
maeneo yalihofadhiwa,”alisema dkt Mahenge.
Amewataka wananchi kuzingatia taratibu na sheria pindi wanapotaka kuanza ujenzi ili kulipanga vyema jiji hilo.
Awali
Mkurugenzi wa Jiji hilo Godwin Kunambi amesema magari hayo wamenunua
kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina yao na baraza la madiwani.
“Haya
magari matatu,double cabin mbili ni sh mil 92,nah ii Toyota hard top ni
sh milioni 160,fedha hizi ni mapato ya ndani na jambo hili linafanyika
kwa jiji hili tu,zamani ilikuwa mpaka uombe serikali kuu lakini sasa
tumenunua kwa mapato yetu wenyewe,”alisema Kunambi.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akijaribu moja ya gari lililonunuliwa na Halmashauri ya jiji la Dodoma kwa ajili ya kuimarisha Kitengo cha udhibiti wa ujenzi holela. |
Amesema
jiji limeona liimarishe kitengo chao cha udhibiti wa ujenzi holela kwa
kununua vitendea kazi hivyo wakiwa wanaamini kuwa vitawarahisishia
katika utendaji wa kazi kwenye Idara ya Ardhi, kutekeleza Mpango kabambe
wa jiji la Dodoma, lengo likiwa ni kuendelea kupima kwa haraka maeneo
yanayokua kwa kasi.
“Jiji
la Dodoma lina km za mraba 2,700 yaani mkoa wa Dar es salaam unaingia
mara mbili kwa jiji la Dodoma kwa kuwa una km za mraba 2,500 hapo hapo
bahari na nchi kavu,lakini jiji la Dodoma ndio pekee limepangwa kwa
asilimia 100,lina mpango kabambe unaoonyesha hakuna sehemu ambayo
haijapangwa,”alisema Mkurugenzi huyo.
No comments:
Post a Comment