 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu
iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya
Mlimani Chato mkoani Geita leo tarehe 10/04/2020.

Rais Dkt. John Magufuli
ameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki katika Parokia ya Mlimani, Wilaya ya
Chato Mkoani Geita kusali Ibada ya Ijumaa Kuu iliyoongozwa na Padre Prof.
Innocent Sanga kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya.
Ibada ya Ijumaa Kuu
huadhimishwa ikiwa ni kumbukumbu ya kusulubiwa na kufa kwa Bwana Yesu Kristo,
zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu
iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya
Mlimani Chato mkoani Geita tarehe 10/04/2020.
|
Katika salamu zake,
Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Padre Sanga kwa mahubiri yaliyowakumbusha
Wakristo kuwa msalaba unaokoa, na kwamba kupitia msalaba Mungu ataikoa dunia
dhidi ya majanga mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na
virusi vya Corona (Covid-19).
Mhe. Rais Magufuli
amesema mpaka sasa idadi ya Watanzania waliothibitika kuwa na virusi vya Corona
ni takribani 29, Watanzania 5 waliopatwa na maambukizi wamepona, Watanzania 3
wamefariki dunia na kwa takribani asilimia 90 ya waliopatwa na virusi hivyo
wanaendelea vizuri.
 |
Padre Innocent Sanga akiongoza Ibada ya Ijumaa
Kuu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani
Chato mkoani Geita tarehe 10/04/2020.
|
Amebainisha kuwa
kutokana na madhara ya ugonjwa huo duniani, upo uwezekano wa kutokea upungufu
wa chakula, hivyo ametoa wito kwa Watanzania kuzalisha chakula cha kutosha na
pia amewataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi kila mahali walipo huku
wakichukua tahadhari za kutoambukizwa kama wanavyoelekezwa na wataalamu.
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki
la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita
tarehe 10/04/2020 katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
|
Rais Magufuli
amesisitiza kuwa Serikali imeamua kutowazuia watu ndani ya nyumba zao wala
kufunga mipaka kwa kutambua madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kutokana na
kufanya hivyo ndani ya nchi na kwa nchi 8 ambazo zinategemea kupata huduma na
bidhaa kupitia Tanzania hususani Bandari ya Dar es Salaam.
Amewataka Watanzania
wote kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ili aiepushe dunia na janga la ugonjwa
wa Corona.
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki
la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita
tarehe 10/04/2020 katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
|
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki
la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita
tarehe 10/04/2020 katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
|
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki
la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita
tarehe 10/04/2020 katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
|
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Padre Innocent Sanga
watatu kutoka kushoto mara baada ya Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi Parokia ya Mlimani Chato mkoani
Geita tarehe 10/04/2020.
|
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka Kanisani katika Ibada
ya Ijumaa Kuu iliyofanyika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana-Maria Mzeyi
Parokia ya Mlimani Chato mkoani Geita tarehe 10/04/2020.
|
No comments:
Post a Comment