Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza na Watendaji na
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba jana, wakati akikagua jengo
la maabara ya Hospitali ya wilaya iliyopo Old Kiomboi katika ziara yake
ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge, akisisitiza jambo wakati
akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba
jana.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula, akisoma taarifa ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya wilaya hiyo.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Iramba wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Makofi yakipigwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi akizungumza kwenye kikao hicho.
Dkt.Mahenge
(katikati) akipokea taarifa ya ujenzi wa Maabara ya Hospitali ya Wilaya
ya Iramba kutoka kwa Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Hussein Sepako
(kushoto) wakati alipofika kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo wakiwa nje wakati wa ziara hiyo.
Mhasibu wa mapato wa wilaya hiyo, Optatusy Ottolikiliwike, akitoa maelezo ya ukusanyaji wa mapato kwenye mnada wa Igumo.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza na wananchi
alipotembelea Mnada wa Igumo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Iramba,
Linno Mwageni na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula.
Mkazi wa Iramba, Lutha Nathaniel, akimpongeza mkuu wa mkoa kwa kufanya ziara katika wilaya hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza na Mjasiriamali
alipotembelea Mnada wa Igumo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba,
Emmanuel Luhahula.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge akizungumza na watendaji wa
wilaya hiyo alipotembelea Mnada wa Igumo. Kulia ni Askari Polisi
wakiimarisha ulinzi eneo hilo. Katikati ni Mkurugenzi wa Wilaya ya
Iramba, Linno Mwageni.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge, akipata maelezo ya Mradi wa Maji uliopo Kijiji cha Kyalosangi Kinampanda..
Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Iramba, Mhandisi Ezra Mwacha, akitoa taarifa ya mradi huo kwa mkuu wa mkoa.
Mwonekano wa tenki la maji la mradi huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge, akiagana na Watendaji na
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba baada ya kumaliza ziara
yake hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUUwa
Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge amewataka watendaji wa
halmashauri kusimamia ipasavyo vyanzo vya mapato vilivyopo kwenye maeneo
yao.
Mahenge
alitoa agizo hilo jana wilayani Iramba mkoani hapa katika muendelezo wa
ziara zake za kutembelea halmashauri zote kwa ajili ya kukagua miradi
ya maendeleo na kuzungumza na watumishi, watendaji na wananchi.
Alisema
anataka viongozi hao hasa watendaji kujua kuwa kupata mapato makubwa
sio lazima kuwa na vyanzo vikubwa kama madini na miradi ya mashamba bali
ni hivihivi vidogo vilivyopo ambapo vikisimamiwa vizuri vitazifanya
halmashauri kupata mapato yakutosha.
"Nataka
watendaji na viongozi wenzangu wajue kwamba mnada ni chanzo kizuri sana
cha mapato hivyo kitiliwe maanani, kuna dhana kuwa ili kupata mapato
makubwa ni lazima kuwepo na miradi mikubwa na vitu vingine vinavyofanana
na hivyo hapana hivi hivi vidogo vikisimamiwa vitafanya mambo makubwa,"
alisema Mahenge.
Dkt.Mahenge
alisema katika ziara yake hiyo wilayani humo aliamua kutembelea mnada
ikiwa ni chanzo mojawapo cha mapato ambacho kimsingi kinajumuisha watu
wengi sana.
Aliyata
makundi hayo ya watu kuwa ni wachoma nyama, wauza nguo,mifugo na
makundi mengine na kuwa alichojifunza ni kutokuwepo kwa usimamizi mzuri
wa ukusanyaji wa mapato licha ya kuwepo kwa makundi hayo.
"
Nimejifunza hatuna usimamizi mzuri na kuwa chanzo hicho kipokipo tu
kwa sababu hayupo mtu anaye hakiki upatikanaji wa mapato kama yamepanda
au kushuka na kwanini makusanyo yana kuwa yale yale kila wakati.
Alisema
katika minada aliyoitembelea amebaini kutokuwepo kwa utaratibu wa kuwa
sajili wanunuzi wa mifugo kwenye eneo moja badala yake kila mtu anafanya
kivyake jambo linalosababisha upotevu wa mapato.
Dkt.
Mahenge alisema kukosekana kwa usimamizi mzuri wa mapato katika maeneo
hayo kunasababishwa na baadhi ya watendaji wa serikali ambao sio
waaminifu ambao wamechangia kutotumika kwa maeneo yaliyotengwa kwa
shughuli za ununuzi na uuzaji wa mifugo na badala yake kwa kushirikiana
na wanunuzi hao wamekuwa wakifanyia shughuli hizo nje ya maeneo hayo.
Aidha
alisema jambo kubwa analolihitaji ni usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa
mapato kwenye mifugo na kwa wafanyabiashara wengine ambao wanafanya
shughuli za kibiashara kwenye eneo hilo la mnada ambao wengi wao hawana
vitambulisho vya ujasiriamali hivyo ametaka kuongezwa kasi ya utoaji wa
vitambulisho hivyo kwani wananchi wako tayari lakini hawajapa fursa ya
kuvipata.
Alizitaka
timu za ukusanyaji wa mapato za halmashauri kunapokuwa na minada kwenda
kujionea ukusanyaji wa mapato badala ya kumuachia mtu mmoja ambaye
anaweza kurubuniwa na kusababisha upotevu wa mapato.
Dkt.Mahenge
katika ziara yake alitembelea na kukagua ujenzi wa jengo la maabara
hospitali ya wilaya ambapo hakuridhishwa na gharama halisi zilizotumika
kwa ujenzi huu kuanzia msingi hadi hatua ya linta na kumwagiza mkuu wa
wilaya hiyo kufanya uchunguzi.
Aidha alikagua ukusanyaji wa mapato katika Mnada wa Igumo na mradi wa maji uliopo Kijiji cha Kyalosangi.
No comments:
Post a Comment