![]() |
Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage, |
NA MARIAM MZIWANDA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, (NEC) imekutana na wawakilishi wa vyama vya Siasa nchini na kuwahakikishia kuwa mpango wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili utafanyika April 17 kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu kutokana na mlipuka wa ugonjwa wa Corona.
Kutokana na hatua hiyo vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo katika zoezi la uandikishaji vimeandaliwa kuanzia tareh 17 hadi 19
Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage, alisema ni muhimu wawakilishi hao kuelewa mpango wa tume wa kuweka wazi daftari la awali la wapiga kura na kuwapa taarifa ya namna Tume hiyo ilivyojipanga kwa ajili awamu ya pili ya uandikishaji.
Aliwahakikishia wawakilishi hao kuwa uchaguzi kwa mwaka huu utakuwa huru na haki na kutokana na maandalizi mazuri yanayoendelea ni wazi utekelezaji wa matumizi utazingatia kifungu 122 cha sheria.
“ Bajeti yetu iko vizuri zaidi ya Bilioni 324 zitatumika ambapo kwa mwaka huu wa fedha tumepatiwa sh bilioni 180 na mwaka jana wa bajeti sh bilioni 144,”alisema.
Alisema ongezeko hilo la bajeti kutoka sh bilioni 273 zilizotengwa uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 zitawezesha maandalizi hayo ikiwemo kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa corona uliopobkwa kuwa na vifaa vya kutosha.

No comments:
Post a Comment