Kauli hiyo imetolewa na Mhe Kitila Mkumbo, Waziri wa Viwanda na Biashara alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) leo tarehe 21 Aprili, 2021 mkoani Dar es Salaam.
“Unaweza kukuta kwenye kampuni wamegombana kutokana na hisa au mmoja anataka kuzidisha hisa kwenye kampuni kinyemela, hayo yatatuliwe kisheria na kikanuni na sio kutumia busara sana ili kuweza kupunguza migororo mingi” amesema Mkumbo
Pia, Mhe Mkumbo ametoa wito kwa wafanyabiashara kuwa na muamko wa kusajili biashara kwasababu kurasimisha biashara inaanza na kusajili, hivyo Watanzania na Wafanyabiashara waitumie Brela katika kurasimisha biashara ili wapate faida za kutambulika wanapofanya biashara na uzuri taratibu za urasmishaji umerahisishwa kwa njia ya mtandao
Pia, Mhe Mkumbo amesema kuwa taasisi ya Brela imepewa jukumu la kuwezesha ufanyaji biashara nchini na sio kudhibiti biashara, hivyo katika utekelezaji wa majukumu amewaelekeza watumishi wa Brela kila wanapopokea taarifa kutoka kwa mfanyabaishara kutaka kufunga biashara au kampuni afuatiliwe kwa ukaribu ili kujua changamoto iliyopelekea kufungwa kwa kampuni hiyo,
“Kama taasisi yenye jukumu kubwa tusione sifa kumhudumia mfanyabiashara anayetaka kufunga biashara labda ufungaji huo utokane na migogoro ndani ya kampuni” amesisitiza Mhe Mkumbo
Nae, Afisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Bw Godfrey Nyaisa amesema kuwa hadi sasa kwa mwaka huu wa fedha, kampuni zilizosajiliwa ni 7148 na malengo ya taasisi ni kufikia usajili wa makampuni 9528 ambapo hadi sasa usajili umefikia asilimia 75 ongezeko hili limetokana na matokeo ya uboreshaji wa mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao
Bw Nyaisa ameeleza kuwa kwa sasa usajili wa kampuni unakamilika ndani ya siku moja, changamoto hutokea endapo anayesajili amewasilisha nyaraka zenye kutiliwa mashaka na wataalam kutoka kwetu au kuwasilisha nyaraka zisizokamilika
Pamoja na kuongea na wafanyakazi Mhe Kitila Mkumbo ametembelea jengo jipya linalotarajiwa kuwa makao makuu ya Brela, ukarabati wa jengo linategemea kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2021
No comments:
Post a Comment