Mazungumzo
hayo yamefanyika leo Aprili 22, 2021 katika Ofisi za TBC Jijini Dodoma
ambapo wamegusia mambo kadhaa ya kuendeleza Wizara na taasisi zake
kimkakati ili kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi, teknolojia na
uchumi duniani.
Waziri Bashungwa alimshukuru Mhe.Balozi kwa
Jitihada walizozifanya kujenga Uwanja wa Taifa uliopewa jina la Uwanja
wa Benjamin Mkapa na kumuomba Balozi kujenga Uwanja mwingine mkubwa
Kanda ya Ziwa ili kumuenzi Hayati John Pombe Magufuli.
Kuhusiana
na Tasnia ya Filamu nchini, Waziri Bashungwa amemuomba Mhe. Balozi
kuweza kusaidia kujenga maktaba ya vifaa vya filamu nchini ambayo
itakuwa katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
Amesema, maktaba hiyo
itawasaidia wazalishaji Filamu nchini kuwa na kuweza kuazima na
kurudisha vifaa tofauti na sasa ambapo kila mmoja anahangaika kutafuta
vifaa peke yake na kwa gharama kubwa.
Pia alimuomba Mhe. Balozi
kuutangaza Utamaduni wa Tanzania nchini mwao na sehemu mbalimbali
duniani kwa kuwa nchi ya China imepiga hatua kubwa kwenye eneo la
sayansi na teknolojia.
Kwa upande wake, Balozi wa China nchini
Mhe Wang Ke amempongeza Waziri Bashungwa kwa Kuteuliwa tena na kuaminiwa
na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumpa nafasi ya kuongoza tena
Wizara hiyo na kuahidi kushirikiana naye.
Mhe. Balozi Wang
ameahidi kufanyia kazi maombi yote aliyotoa Mhe. Bashungwa ambapo
amesema atajadiliana na Serikali yake ili kuona ni kwa namna gani
wanaweza kushughulikia maombi hayo.
Balozi Wang amemuomba Waziri
Bashungwa kuweka karibu ushirikiano wa TBC na Kampuni ya Star Times
nchini ili kuweza kuimarisha Sekta ya Habari hapa nchini.
Ameipongeza Tanzania kwa kuwa miongoni mwa nchi iliyoiunga mkono nchi ya China katika kuandaa Michuano ya Olimpiki 2008.
Balozi
Wang ametoa fursa za nafasi za mafunzo kwa watumishi wa Serikali
nchini China ili kuweza kuongeza ujuzi wa kuhabarisha jamii kiujumla.
Tanzania imekuwa na ushirikiano wa karibu na wa muda mrefu na nchi ya China ambao umekuwa wa kihistoria tangu kipindi cha uhuru wake chini ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
No comments:
Post a Comment