Matokeo chanyA+ online




Wednesday, May 18, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akizungumza jana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati akifungua wiki ya michezo ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida  iliyoanza juzi mkoani hapa. 

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa wiki hiyo ya michezo. 
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akipiga mpira wakati wa ufunguzi huo. 

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, akiwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi hiyo. Kulia ni Meneja wa TIA Kampasi ya Singida Dk.James Mrema.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, akikagua timu katika ufunguzi huo. 
Mazoezi ya viungo yakifanyika.
Mazoezi yakiendelea.
Mazoezi yakiendelea.
Mazoezi yakiendelea siku ya kwanza ya tamasha hilo la michezo.
Mazoezi yakifanyika.
Jogging ikifanyika.
Mashabiki wakifuatilia michezo iliyokuwa ikifanyika.
Michezo ikiendelea.
michezo ikiendelea.
Kivumbi kikitimka wakati wa michezo hiyo.

Mazoezi yakifanyika.
Timu    zikiingia uwanjani.
Picha ya pamoja.
Mchezo wa Netball ukifanyika.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Singida Golden Marathon ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Singida Golden Runners , Raymond Msangi akizunguza wakati wa uzinduzi wa Singida Golden Marathon uliofanyika juzi Viwanja vya Peoples mjini hapa  ambao ulifanyika sanjari na kuanza mazoezi ya Jogging kuelekea kilele cha mbio hizo zitakazofanyika Julai 23, 2022..
Katibu wa Singida Golden Mrathon Nemes Mushi akizungumza kwenye uzinduzi huo 
Washiriki wa mazoezi hayo wakijiandaa kwa kufanya jogging.
Wadau wakiwa viwanja vya Peoples wakati wa uzinduzi huo.
Mazoezi yakifanyika kabla ya kuanza kukimbia kilometa tano.

Friday, May 6, 2022

ANWANI ZA MAKAZI KUWEZESHA ZOEZI LA SENSA KIDIJITALI



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Khamis Abdulla akizungumza na watendaji wa mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa kikao chake na watendaji hao kupokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi katika mkoa huo.

    Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 
   Mhe. Mohamed Khamis Abdulla akiagana na baadhi ya watendaji wa 
   mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kikao chake na watendaji hao 
    kupokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi katika mkoa huo.



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Khamis Abdulla (Kulia mwenye suti) akikagua nguzo ya barabara ya Mwera Pogwe na Mtaa wa Tunguu wa mkoa wa Kusini Unguja wakati wa kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi katika mkoa huo.





MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MWAKILISHI WA UNHCR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 6 Mei 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) hapa nchini Mahoua Parums, mazungumzo yaliofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

 

Katika mazungumzo hayo Bi. Mahoua Parums amesema Tanzania imeendelea kuwa nchi muhimu zaidi kwa Shirika la kuwahudumia wakimbizi pamoja na wakimbizi wenyewe kutokana na kuwa nchi iliopokea  idadi kubwa ya wakimbizi kwa miongo kadhaa. Ameongeza kwamba mchango wa Tanzania katika kupokea na kuhudumia wakimbizi hautasahaulika ikiwa ni pamoja na ukarimu wanaopata wakimbizi mahali wanapofikia.

 

Bi. Parums amesema anafurahi kuwa katika nchi ambayo ina umoja na mshikamano na mataifa mengine wakati wa kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo za wakimbizi.

 

Makamu wa Rais Dkt. Mpango amemkaribisha Mwakilishi huyo mkazi hapa nchini na kumuahidi kwamba serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) hapa nchini.

 

Aidha ameongeza kwamba Tanzania imekua mstari wa mbele katika kutafuta muafaka wa amani na utulivu katika nchi zinazokumbwa na migogoro mbalimbali ikiwemo vita ili kupunguza idadi ya wakimbizi wanaokimbia nchi hizo. Amesema kinachohitajika ni kuhakikisha kunapatikana suluhu za kudumu katika mataifa yaliokumbwa na migogoro ili wakimbizi hao wapate kurudi katika nchi zao na kushiriki katika shughuli za maendeleo katika nchi hizo.

 

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Jumuiya ya Madola wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mheshimiwa Patricia Scotland, mazungumzo yaliofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.




 

Thursday, May 5, 2022

KILO 22,800 ZA MATUNDA YA PARACHICHI KUTOKA TANZANIA ZAWASILI INDIA KUFUNGUA SOKO KUBWA LA ZAO HILO NCHINI HUMO

 

Tarehe 4 Mei 2022 ni siku adhimu ambapo kwa mara ya kwanza Ubalozi wa Tanzania nchini India, umepokea Kontena la maparachichi kutoka Tanzania kupitia Kampuni ya IG Fruits ya nchini India. Mapokezi haya yamefanyika katika Bandari ya Jawaharlal Nehru Mumbai.
 
‘Naomba kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu maparachichi tuliyoyapokea leo ni Kontena la futi 40 ambalo ndani yake lina trays za parachichi 5,700. Na kila tray moja lina uzito wa kilo 4. Huko nyuma tuliwahi kupokea shehena ya kilo 200 ambayo ilikuja na ndege yetu ya ATCL’ - Balozi Anisa K Mbega
 




 

Tuesday, May 3, 2022

 Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mei 3 , 2022 amejumuika pamoja na Wananchi  katika Baraza la Eid El Fitri lililofanyika katika Ukumbi wa   Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNICC) Mkoa wa Dar es Salaam.


Baraza la Eid Al Fitri  hufanyika kila baada ya  kukamilika kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani








                                                                  Eddi Mubaarak

Balozi David Concar speaks in #Arusha“As a diplomat who was once a journ...

Zlatan Milišić- Without freedom of the press, there is no freedom.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliofanyika Jijini Arusha