Matokeo chanyA+ online




Saturday, January 13, 2018

KILELE CHA SHEREHE YA MAPINDUZI    ZANZIBAR JANUARY12, 2018

 

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasalimia Wananchi waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalioadhimishwa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kuhudhuria sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwa katika msafara maalum wa mapikipiki.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipokea salamu na kupigwa mizinga 21 wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalioadhimishwa katika Viwanja vya Amaan Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua bwaride Maalum la maadhimisho ya Sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalioadhimishwa katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
  • BAADHI ya Wananchi na Wageni waalikwa wakihudhuria maadhimisho ya sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika katika Viwanja vya Amaan Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akikagua bwaride Maalum la maadhimisho ya Sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalioadhimishwa katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
  • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi wa Jukwaa Kuu wakisimama wakati wa kutowa salamu na kupigwa mizinga 21 kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya sherehe za kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
  • MABALOZI wanaowakilisha Nchini zao Tanzania wakiwasili katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kuhudhuria sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar 
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi D.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Rais Mstahafu Tanzania Dk. Gharib Bilal wakatia alipowasili kwenye kilele cha sherehe za Mapinduzi Zanzibar kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein Akisaliniana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika viwanja vya Amaan, kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu alipowasili katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kuhudhuria sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
  • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Fatma Karume Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar alipowasili katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kuhudhuria sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
  • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akisamiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete alipowasili katika viwanja vya Amaan, kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume, alipowasili katika Uwanja wa Amaan kuhudhuria hafla ya sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • RAIS Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakati akiwasili katika Viwanja wa Amaan Zanzibar kuhudhuria sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.
  • MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samiha Suluhu Hassan akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu alipowasili katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khatib wakati akiwasili katika viwanja vya Amaan kuhudhuria sherehe za kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • WAZIRI Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi wa Tanzania wakati akiwasili katika viwanja vya amaan Zanzibar kuhudhuria sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar
  • MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa wakati akiwasili katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
  • Kikosi cha Bendera kikipita na kutowa heshima wakati wa kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • GWARIDE la JWTZ likipita kwa mwendo wa kasi na kutowa heshima kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.wakati gwaride la kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • GWARIDE la JWTZ likipita kwa mwendo wa kasi na kutowa heshima kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.wakati gwaride la kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • GWARIDE la JWTZ likipita kwa mwendo wa kasi na kutowa heshima kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.wakati gwaride la kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • MABALOZI wa Nchini mbalimbali wanaowakilisha Nchini zao Tanzania wakifuatilia sherehe za Maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
  • PICHA NA IKULU ZANZIBAR

Tuesday, January 9, 2018

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWAS...

KILA MMOJA KWA NAFASI ULIYOPO KATIKA TAIFA HILI WAJIBIKA KWA MAARIFA YAKO YOTE "CHAPA KAZI"





RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASSA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JANUARI 9,2018.

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2018. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada yakumaliza mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa  Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimfungulia mlango Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2018.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.Januari 9,2018.
PICHA NA IKULU

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE. DOTTO MASHAKA BITEKO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JANUARI 8,2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimmkabidhi nyenzo za kazi Mhe. Dotto Mashaka Biteko baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakimsikiliza  Mhe. Dotto Mashaka Biteko akila kiapo cha  Uadilifu cha Viongozi wa Umma baada ya kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakimsikiliza  Mhe. Dotto Mashaka Biteko akiongea machache  baada ya kuapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kumuapisha Mhe. Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Mhe. Dotto Mashaka Biteko baada ya kumuapisha kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mhe. Dotto Mashaka Biteko  baada ya kumuapisha  kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Januari 8, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kumuapisha  Mhe. Dotto Mashaka Biteko  kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Januari 8, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kumuapisha  Mhe. Dotto Mashaka Biteko  kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Januari 8, 2018.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini waliohudhuria kwenye hafla ya kuapishwa  Mhe. Dotto Mashaka Biteko  kuwa Naibu Waziri wa Madini katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Januari 8, 2018
PICHA NA IKULU

Tuesday, January 2, 2018

RC.MNDEME AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA RUHUHU WILAYANI NYASA LEO,AMPA MKANDARASI MIEZI 6 KUMALIZA UJENZI WA DARAJA








TRA Yatoa Utaratibu wa Kusajili Walipa Kodi Wadogo


Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya  (kulia)akizungumza  na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa Kampeni ya Usajili wa Walipakodi.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeondoa utaratibu wa awali kwa walipakodi wadogo kulipia kodi kabla ya kuanza kufanya biashara na badala yake kuwataka kulipia robo ya kwanza ndani ya siku tisini tangu kusajiliwa.

Kamishna wa Kodi za Ndani, Elijah Mwandumbya ameyabainisha  hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Kampeni ya Usajili wa Walipakodi.

Mwandumbya amesema  jukumu la usajili wa walipakodi kwa Mamlaka hiyo ni chanzo cha kuongeza idadi ya walipakodi, wigo wa ulipaji kodi, kuongeza makusanyo pamoja na kuwa na taarifa sahihi za walipakodi wanaostahili kukadiriwa na kutozwa kodi ili kuchangia Pato la Taifa.

“kampeni hii inaenda sambamba na mabadiliko makubwa tuliyoyafanya kwa walipakodi wadogo kwa kuwapa siku tisini za kulipa kodi kwa robo ya kwanza ya malipo pindi tu watakapokuwa wamesajiliwa hivyo mabadiliko hayo yatakuwa chachu katika usajili kwani tunatarajia kusajili walipakodi takribani milioni moja nchi nzima,”alisema Mwandumbya.

Kamishna wa Kodi za Ndani amesisitiza kuwa usajili wa TIN ni bure na utafanyika katika ofisi zote za Mamlaka hiyo na katika vituo maalum vitakavyokuwa vimeteuliwa na kutangazwa kupitia vyombo vya habari na matangazo katika maeneo husika.

Aidha, Mwandumbya amewataka wananchi kujihadhari na vishoka wanaoweza kutumia mwanya wa kuharibu nia njema ya kampeni hiyo kwani hakuna wakala yeyote aliyepewa jukumu la kusajili wala kutoa fomu za usajili wa zoezi hilo.

Amefafanua kuwa muhusika lazima aende mwenyewe ili apigwe picha na kuchukuliwa alama za vidole pia atatakiwa aende na mkataba wa pango au uthibitisho wa umiliki wa mahali pa biashara, barua yenye muhuri na namba ya simu ya Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa pamoja na kitambulisho cha muhusika kama vile hati ya kusafiria, leseni ya udereva, kitambulisho cha uraia au cha mpiga kura.

Kampeni hiyo imezinduliwa nchi nzima kwa nia ya kuhakikisha kila mwananchi anayestahili kupatiwa namba ya utambulisho ya mlipakodi anasajiliwa na kupata namba hiyo kwa urahisi na haraka.