Matokeo chanyA+ online




Sunday, February 11, 2018

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MUFINDI

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Iringa ambapo leo alitembele wilaya ya Mufindi na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ikiwa mmoja ni wa kujenga maabara ya kisasa na madarasa na kidato cha tano na cha sita katika Sekondari ya Mgololo na upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.
Akiwahutubia wananchi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi  la Upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole , Makamu wa Rais alisema katika kila kituo cha afya kinachopanuliwa ama kujengwa Serikali imezingatia  huduma za mama na mtoto ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto, kuborsha huduma za upasuaji .
Serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho na kutumia mafundi wa kawaida kujenga ilikuweza kusaidia kutoa ajira kwa vijana zaidi wa eneo husika.
Makamu wa Rais amezitaka halmashauri zisimamie utoaji na matumizi ya fedha wanazotoa kwa Vijana asilimia 5 na Wanawake asilimia 5 ili kuleta tija kwenye shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais alisema  “tunapozungumzia uchumi wa viwanda lazima tuwaandae Vijana tangia wadogo, tuhakikishe wanafundishwa  yale yanayohitajika”.
Makamu wa Rais aliwaambia wakazi wa Mafinga, watakapokuja tena kwenye kampeni watawataka wananchi waseme Serikali yao imewafanyia nini.
Mapema leo Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa  ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Mgololo, ujenzi ambao utagharimu  shilingi milioni  450 za kitanzania chini ya ufadhili wa kiwanda cha Mufindi Paper Mills.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa ujenzi wa kituo cha afya Ihongole Mafinga, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma maneno yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Mgololo, Mufindi mkoani Iringa mara baada ya kulifungua ,pembeni yake ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Rai wanaomiliki kiwanda cha Mufindi Paper Mills Bw. Jaswant S. Rai na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza. 





 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwenye uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole

Saturday, February 10, 2018

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA ASEMA MWISHO WA KERO ZA ARDHI NA DHURUMA NYINGI KWA WANYONGE UMEFIKA



MAKAMU WA RAIS KATIKA SIKU YA PILI WILAYA YA KILOLO MKOANI IRINGA
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah akisoma taarifa ya wilaya yake mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati ziara ya Makamu wa Rais wilayani Kilolo



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Wilaya ya Kilolo ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkoani Iringa, wengine pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto (kulia) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas

Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mhe. Venance Mwamoto akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Utawala la Shule ya Sekondari Kilolo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka mkoa wa Iringa Ndugu Salim Abri Asas akihutubia wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya Sekondari Kilolo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa jengo la Utawala la Shule ya Sekondari ya Kilolo


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa B. Amina Masenza wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Utawala la shule ya sekondari ya Kilolo mkoani Iringa

MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI IRINGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa wodi katika zahanati ya Kising’a mkoani Iringa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya GBRI inayozalisha bidhaa za mboga mboga zinazojulikana kama Eat Fresh mjini Iringa.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa baadhi ya bidhaa za mboga mboga za Eat Fresh na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GBRI Bi. Hadija Jabir

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Kising’a  tayari kwa ufunguzi wa wodi katika Zahanati ya Kising’a. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya uendeshaji na uzalishaji wa kiwanda cha Ivori Food & Bevarage cha Iringa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Suhail Esmail Thakore.



Thursday, February 8, 2018

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE WA SHIMUTA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bw. Khamis Mkanachi ambaye aliongozana na Uongozi na Wajumbe wa Shirikisho kukutana na Makamu wa Rais kwenye makazi yake, Kilimani mjini Dodoma


 
  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania kwenye makazi yake Kilimani mjini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Shirikisho la Michezo la Mashirika ya umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania mara baada ya kumaliza mazungumzo kwenye makazi yake Kilimani, mjini Dodom

PASPOTI NI HAKI YAKO .PASIPOTI NI WAJIBU WAKO