Matokeo chanyA+ online




Monday, July 11, 2022

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA WANFUNZI-DIASPORA WA MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani wanaofundisha na kusoma vyuo mbalimbali vya Marekani ambao wapo nchini kwa ziara ya kikazi hadi tarehe 17 Julai 2022.

Ziara hiyo iliyoratibiwa na Mtanzania-Diaspora, Bi Zawadi Sakapala ambaye ni mmiliki wa kituo cha “Community Centre” kilichopo Kijichi jijini Dar Es Salaam inalenga pamoja na mambo mngine, kutoa fursa kwa wanafunzi hao kujifunza masuala ya utamaduni wa Tanzania na kubadilishana ujuzi na uzoefu katika masomo ya sayansi, ufundi, ufundishaji na Usimamizi wa watoto wadogo (daycare).

Katika kikao hicho, Bi Zawadi alimfahamisha Mhe. Balozi Mulamula kuwa kituo chake kimekuwa kikishirikiana na vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani kuratibu ziara za walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani kutembelea nchi za Afrika kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika sekta ya elimu.

Hivyo, ili kuimarisha sekta ya elimu katika nchi za Afrika, kikao hicho kiliazimia kuongeza jitihada za kuhamasisha Waafrika wengi zaidi kujiunga na vyuo vya Marekani, kuunganisha vyuo vya Afrika na Marekani, wanafunzi-Watanzania wanaopata fursa ya kusoma Marekani, watumike kufundisha lugha ya Kiswahili ikiwa ni moja ya njia ya kueneza lugha hiyo duniani pamoja na kwahimiza watu wenye asili ya Afrika kutumia elimu, ujuzi na maarifa waliyopata wakiwa ughaibuni kuinua jamii za nchi za Afrika.

Wakati huo huo, Balozi Mulamula amekutana na Ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya Maendeleo (UNDP) ambao upo nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo na wadau wa siasa ili kubainisha maeneo ambayo, shirika hilo linaweza kusaidia katika uendeshaji wa uchaguzi mkuu ujao.

Ujumbe huo unaongozwa na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani ya Umoja wa Mataifa, Bw. Akinyemi Adegbola umefanikiwa kufanya vikao na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wawakilishi wa vyama vya siasa na asasi za kiraia, umepokea maoni ya wadau hao ya maoneo yanayohitaji msaada na umeahidi utayafanyia kazi kikamilifu. Maeneo hayo ni pamoja na uelimishaji wa wapiga kura, msaada wa kiufundi katika upigaji na uandikishwaji wa wapiga kura na teknolojia ya mawasiliano wakati zoezi la uchaguzi.

Kwa upande wake, Balozi Mulamula aliueleza ujumbe huo kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kipindi kifupi cha uongozi wake ameonesha dhamira ya dhati ya kuboresha mazingira ya kisiasa nchini, kwa kuhamasisha majadiliano ya kisiasa, ushirikishwaji wa wadau wote, umoja na mshikamano wa kitaifa. Hivyo, aliuhakikishia ujumbe huo kuwa uchaguzi ujao utaendelea kuwa huru, haki na amani kama ilivyo desturi ya Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani (hawapo pichani) wanaosoma na kufundisha vyuo mbalimbali vya Marekani ambao wapo nchini kwa ziara maalum hadi tarehe 17 Julai 2022.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza mmoja wa mwanafunzi anayesoma katika vyuo vikuu vya Marekani kuhusu mikakati ya kusaidia vijana wa Afrika kupata elimu bora itakayoweza kukabili mazingira ya dunia ya sasa.

Mhitimu wa Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Howard cha nchini Marekani ambaye pia ni Kiongozi wa Taasisi ya 3GC Inc. akieleza shughuli za taasisi hiyo zinazolenga kuwasaidia vijana wa Afrika 
Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga wakifuatilia mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani wanaosoma na kufundisha vyuo mbalimbali vya Marekani


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimvisha scurf ya bendera ya Tanzania, mmiliki wa kituo cha “Community Centre” kilichopo Kijichi jijini Dar Es Salaam, Bi. Zawadi Sakapala

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani wanaosoma na kufundisha vyuo mbalimbali vya Marekani



BALOZI MULAMULA AKUTANA NA  AFISA UCHAGUZI MKUU WA UN


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani ya Umoja wa Mataifa, Bw. Akinyemi Adegbola yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam

Baadhi ya ujumbe uliongozana na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani ya Umoja wa Mataifa, Bw. Akinyemi Adegbola kwenye mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Afisa huyo.

Ujumbe wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ukifuatilia mazungumzo yake na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani ya Umoja wa Mataifa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiagana na ujumbe wa UNDP ambao upo nchini kwa ajili ya kuzungumza na wadau wa siasa kuhusu uchaguzi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa UNDP ambao upo nchini kwa ajili ya kuzungumza na wadau wa siasa kuhusu uchaguzi.


BALOZI MULAMULA AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UN WOMEN

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa  UN Women, Bi.  Hodan Addou kwenye Hoteli ya Seana jinini Dar Es Salaam.


BALOZI MULAMULA AKUTANA NA  BALOZI MTEULE LT. JEN. MATHEW EDWARD MKINGULE 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule Lt. Jen. Mathew Edward Mkingule yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Balozi Mteule Lt. Jen. Mathew Edward Mkingule baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam


 

PRESIDENT SAMIA SIGNS MOURNING BOOK OF FORMER ANGOLA PRESIDENT, HON. JOSE EDUARDO DOS SANTOS

BENKI YA DUNIA YAIPONGEZA TANZANIA KUWEKEZA KWENYE KILIMO


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisisitiza jambo alipokutana kwa mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa (hayupo pichani), katika kikao kilichofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akizungumza jambo na ujumbe wa Benki ya Dunia ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, (hayupo pichani), katika kikao kilichofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kumaliza kikao chao katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa (wa tano kulia), baada ya kumaliza kikao chao katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam. Wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamisi Shaaban.

Benki ya Dunia imeipongeza Tanzania kwa kuamua kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye maeneo ya uzalishaji kikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi mambo ambayo yatachochea ukuaji wa kipato cha wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki, Bi. Victoria Kwakwa, alipokutana na kufanya mazungumzo rasmi na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Aliahidi kuwa Benki yake na washirika wake wengine watasaidia juhudi za Serikali za kufanikisha mapinduzi katika sekta hizo muhimu kwa kutoa fedha pamoja na ushauri wa kitaalam ili mpango huo wa kuendeleza kilimo, mifugo na uvuvi uwe na tija.

Bi. Kwakwa alisema kuwa changamoto ya UVIKO 19 na vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine vimeibua changamoto kubwa ya uhaba wa mazao ya nafaka na kwamba Tanzania ikijipanga vizuri inaweza kuwa ghala la chakula na kuifanya ijitosheleze kwa chakula na kutoagiza chakula kutoka nje.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa Serikali imeamua kuwekeza fedha kwenye maeneo ya uzalishaji akitolea mfano wa ongezeko la bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 200 hadi zaidi ya shilingi bilioni 900 ili kuiwezesha sekta hiyo kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuzalisha ajira kwa wananchi.

Dkt. Nchemba aliishukuru Benki hiyo kwa uwekezaji wa dola za Marekani bilioni 2.8 katika miradi 11 ya kimkakati iliyowasilishwa katika Benki hiyo katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema kuwa uwekezaji huo utaisaidia nchi kupambana na umasikini pamoja na ukuaji jumuishi wa maendeleo ya watu na kuahidi kuwa fedha zinazopatikana kutoka katika Benki hiyo zinatumika ipasavyo ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa.

Aidha, Dkt. Nchemba, aliishukuru Benki hiyo kwa kuiidhinishia Tanzania kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia mpango mpya wa utoaji mikopo na misaada wa IDA 20 ulioanza kutekelezwa rasmi mwezi Julai, 2022.

Aliiomba Benki hiyo kuharakisha utoaji wa fedha ili miradi iliyopangwa kutekelezwa kupitia mpango huo wa miaka mitatu iweze kutekelezwa na kwamba Serikali itashukuru endapo kiwango hicho cha fedha kitaongezwa ili miradi iliyopo hivi sasa inayokadiriwa kugharimu dola za Marekani bilioni 4.9 iweze kukamilika kwa wakati.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha na Mipamgo, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamisi Shaaban, Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Rished Mohamed Bade na Viongozi wengine kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA BI. VICTORIA KWAKWA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bi. Victoria Kwakwa mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2022.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bi. Victoria Kwakwa mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Julai, 2022.


 

Sunday, July 10, 2022

MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA AWASILI NCHINI KUTETA NA MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimpokea Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere-Dar es Salaam, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Wapili kushoto), Pamoja na maafisa wa Serikali wakiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere-Dar es Salaam, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere-Dar es Salaam, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akisalimiana na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Rished Bade, wakati wa kumpokea Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika Bi. Victoria Kwakwa, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere-Dar es Salaam, aliyewasili kwa ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini.


WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa uhusiano kati ya Serikali na Benki ya Dunia unazidi kuimarika na kwamba watanzania watarajie maendeleo makubwa kupitia ushirikiano huo.

Dkt. Nchemba amesema hayo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kumpokea Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, aliyewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa mwaliko wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuisaidia nchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi ikiwemo ujenzi wa miundombinu, elimu, afya, mazingira na mingine mingi kupitia mpango wa mikopo nafuu wa dirisha la IDA 19 ambao umemaliza muda wake na pia nchi inatarajia kupata fedha nyingine za kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia dirisha jipya la IDA 20.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, amesema kuwa lengo la ziara yake nchini Tanzania ni kujitambulisha na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki hiyo baada ya kuchukua nafasi ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika Dkt. Hafez Ghanem, ambaye amestaafu.

Akiwa nchini, Bi. Kwakwa, anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam, baadae ataelekea Visiwani Zanzibar ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na atakutana pia na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na viongozi wengine kadhaa wa Serikali.


 

SHEIKH MKOA WA SINGIDA ATOA ONYO WAISLAM KUGOMBEA NYAMA, AKEMEA , ULAWITI, UKATILI WA KIJINSIA

Waislam wakiswali Swala ya Idd al- Adha ambayo imefanyika leo katika Msikiti Mkuu wa Taqwa uliopo Manispaa ya Singida.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro, akiongoza Swala ya Idd al- Adha ambayo imefanyika leo katika Msikiti Mkuu wa Taqwa uliopo Manispaa ya Singida.
Isihaka Hassan akitoa hotuba katika swala hiyo.

Saturday, July 9, 2022

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA UENDESHAJI WA BENKI YA DUNIA (IDA) AXEL VAN TROTSENBURG, DAKAR, SENEGAL TAREHE 08 JULAI, 2022

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa uendeshaji wa Benki ya Dunia (IDA) Axel van Trotsenburg, Dakar nchini Senegal kabla ya kuanza mazungumzo tarehe 07 Jullai, 2022.
.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa uendeshaji wa Benki ya Dunia (IDA) Axel van Trotsenburg, Dakar nchini Senegal kabla ya kuanza mazungumzo tarehe 07 Julai, 2022.
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa uendeshaji wa Benki ya Dunia (IDA) Axel van Trotsenburg mara baada ya mazungumzo yao Dakar nchini Senegal tarehe 07 Julai, 2022.

Thursday, July 7, 2022

TANZANIA KUNUFAIKA NA WENYEJI WA MKUTANO WA 65 WA UNWTO

Tanzania inatarajia kunufaika na fursa mbalimbali zitakazotokana na  Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani UNWTO – CAF utakaofanyika jijini Arusha kuanzia

 Oktoba 5 hadi 7, 2022.

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipokua akizungumza na vyombo vya habari  jijini Arusha  kuhusu kufanyika kwa mkutano huo ambapo amesema Tanzania itanufaika  na ujio wa mkutano huo kwa kukuza na kuendeleza utalii, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa pamoja na lengo litakalowekwa la haki ya msingi ya binadamu kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya Utalii bila vikwazo vyovyote.

 

Kuhusu mkutano huo Mhe. Waziri Balozi Pindi  Chana amesema utahudhuriwa na watu mashuhuri wakiwemo Katibu Mkuu wa UNWTO, Mawaziri wa Utalii kutoka nchi Wanachama wa Shirika la Utalii Duniani – Kamisheni ya Afrika na wadau wa utalii kutoka ndani na nje ya Afrika na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.

 

“Mkutano huu utahusisha matukio mbalimbali ikiwemo Mkutano wa Mawaziri wa Utalii kutoka nchi wanachama, Jukwaa la Uwekezaji kwa ajili ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini na  mafunzo kwa wadau wa sekta ya Utalii yaani Marketing Symposium kwa lengo la kuwajengea uwezo wadau wa utalii kuhusu utangazaji Utalii”. Amefafanua  Waziri Chana

 

Aidha, kwa kutambua umuhimu wa mkutano huo, Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa rai kwa wadau wote wa utalii hususan wakazi wa Jiji la Arusha na maeneo ya jirani wanaotoa huduma za malazi, mawakala wa biashara za utalii, na waongoza watalii kuonesha ukarimu wa hali ya juu kwa washiriki wa Mkutano wa 65 wa UNWTO – CAF kwa kipindi chote watakachokuwa hapa nchini ili waitangaze vyema Tanzania.

 

Akizungumza kwa niaba ya UNWTO, Mkurugenzi wa Shirika la Utalii Duniani Kamisheni ya Afrika Bi. Marie Elicie, amesema wameridhishwa na namna Tanzania  ilivyo jiandaa kwa  mkutano huo wa Kimataifa kuanzia viwanja vya ndege, hoteli na ukarimu kwa watoa huduma.



Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Pindi akizungumza Mkurugenzi wa Shirika la Utalii Duniani Kamisheni ya Afrika Bi. Marie Elicie mara baada ya kumaliza kuongea na Waandishi wa Habari.


Wajumbe wa kamati ya Taifa ya maandalizi ya Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani UNWTO – CAF

 

KIGOMA KUTUMIA UMEME WA GRIDI YA TAIFA IFIKAPO AGOSTI 2022



Mashine umba tatu zitakazotumika katika Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Nyakanazi, kwa ajili ya kusabaza umeme wa Gridi ya Taifa katika Mkoa wa Kigoma na mikoa jirani. Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba alifanya ziara ya kukagua kituo cha hicho na njia ya kusafirisha umeme kutoka Mradi wa Rusumo, Julai 6, 2022, mkoani Kagera


Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo cha Nyakanazi, Makampuni ya Wakandarasi waliojenga kituo hicho, Mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, wakati wa ziara ya kukagua kituo cha hicho na njia ya kusafirisha umeme kutoka Mradi wa RUSUMO hadi kituo cha Nyakanazi, Julai 6, 2022, mkoani Kagera

Kazi ya uvutaji wa nyaya za umeme ukiendelea katika nguzo zitazotumika kusafirisha umeme kutoka Mradi wa Rusumo hadi Kituo cha Umeme cha Nyakanazi, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba alifanya ziara ya kukagua kituo cha hicho na njia ya kusafirisha umeme kutoka Mradi wa Rusumo, Julai 6, 2022, mkoani Kagera.


Mafundi wakiendelea na Kazi ya kusimamisha nguzo za umeme zitazotumika kusafirisha umeme kutoka Mradi wa Rusumo hadi Kituo cha Umeme cha Nyakanazi, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba alifanya ziara ya kukagua kituo cha hicho na njia ya kusafirisha umeme kutoka Mradi wa Rusumo, Julai 6, 2022, mkoani Kagera.


Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (wapili kulia) pamoja na ujumbe alioambata nao akiangalia kazi ya usimamishaji wa nguzo za umeme zitazotumika kusafirisha umeme kutoka Mradi wa Rusumo hadi Kituo cha Umeme cha Nyakanazi, wakati wa ziara ya kukagua kituo cha hicho na njia ya kusafirisha umeme kutoka Mradi wa Rusumo, Julai 6, 2022, mkoani Kagera

 

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA SENEGAL JIJINI DAKAR

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Senegal Mhe. Macky Sall tarehe 06 Julai, 2022 kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika zinazonufaika na Dirisha la Maendeleo la Kimataifa (IDA 20 Summit for Afrika) tarehe 07 Julai, 2022 Dakar Senegal.





Wednesday, July 6, 2022

RAIS MHE. SAMIA AWASILI NCHINI SENEGAL

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Leopold Sedar Senghor Jijini Dakar nchini Senegal tarehe 06 Julai 2022 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika zinazonufaika na Dirisha la Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa)