Matokeo chanyA+ online




Monday, February 6, 2023

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. PHILIP MPANGO AKUTANA NA MWANAMFALME WA DUBAI FEB 6 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mwenyekiti wa kampuni ya Blue Carbon LLC ambaye ni  Mwanamfalme wa Dubai Mheshimiwa Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum, alipofika kumsalimia  Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma  tarehe 06 Februari 2023.

 






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa kampuni ya Blue Carbon LLC ambaye ni  Mwanamfalme wa Dubai Mheshimiwa Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum, mara baada ya kufika  Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma  tarehe 06 Februari 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa kampuni ya Blue Carbon LLC ambaye ni  Mwanamfalme wa Dubai Mheshimiwa Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum pamoja na ujumbe aliofuatana nao mara baada ya kufika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma  tarehe 06 Februari 2023.

 



 

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum ambaye ni Mwanafamilia wa Utawala wa Mji wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwanafamilia wa Utawala wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) aliyeambatana na Ujumbe wake Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 06 Februari, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwanafamilia wa Utawala wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 06 Februari, 2023.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwanafamilia wa Utawala wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) pamoja na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 06 Februari, 2023.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwanafamilia wa Watawala wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 06 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi ya Picha ya Jengo la Kihistoria la Zanzibar, Bait el Ajaib, Mwanafamilia wa Utawala wa Dubai kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 06 Februari, 2023.

 



 

RAIS SAMIA ATOA SULUHU MGOGORO WA ARDHI KINGALE - KONDOA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Kingale katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Gereza la King'ang'a ambao wamekuwa kwenye mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miongo mitatu dhidi ya eneo lenye ukubwa wa ekari 7,495.74. Mwishoni mwa wiki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa Suluhu ya mgogoro huo kwa kuzingatia mahitaji ya Wananchi.

 

Wananchi wa Vijiji vya Kingale katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Gereza la King'ang'a wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule mara baada ya kuwasilisha suluhu ya mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miongo mitatu katika eneo lao. Mwishoni mwa wiki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa Suluhu ya mgogoro huo kwa kuzingatia mahitaji ya Wananchi.



RAIS SAMIA ATOA SULUHU MGOGORO WA ARDHI KINGALE - KONDOA 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa Suluhu kwenye mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miongo mitatu dhidi ya eneo lenye ukubwa wa ekari 7,495.74 lililopo katika Vijiji vya Kata ya Kingale katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Gereza la King'ang'a ambalo ni eneo lenye rutuba kwa shughuli za kijamii za uzalishaji.

 

Suluhu hiyo imewasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa niaba ya Mhe. Rais na ameitoa mbele ya wananchi wa Kata hiyo wakiwa na viongozi wao.

 

"Ardhi yote ni mali ya Serikali, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alipofika hapa alifikisha hili jambo kwa Mhe Rais aamue na Rais ametoa suluhu kwa Wanakingale. Amesema eneo lenye mgogoro la ukubwa wa ekari 7,495.74, ekari 3,272.4 zibaki kwa wananchi watumie kwa shughuli za kilimo, mifugo na za kiuchumi na Magereza watachukua ekari zilizobaki" amesema Mhe. Senyamule

 

Mbali na kuwasilisha utatuzi pia Mhe  Rais ameagiza mambo kadhaa yafanyike katika eneo hilo; "Mhe. Rais ameagiza kuwa ndani ya mwezi mmoja, watu wa ardhi waje kuonyesha utaratibu wa maeneo yaliyogawanywa, yapimwe na alama ziwekwe zinazoonekana kwa kila mmoja. Vijiji tuendelee kutunza mipaka kuzuia mwingiliano wa matumizi, Magereza pia mtunze mipaka, wananchi wapo upande wa Bonde linalofaa kwa umwagiliaji. Wizara ya Kilimo mfanye utaratibu wa kujenda mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji, mifungo pia mjenge majosho kwa ajili ya kuosha mifungo ya wananchi" Ameongeza Mhe. Senyamule

 

Kadhalika, Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi hao kufanya maendeleo kwa kushirikiana na Magereza kwani mgogoro umekwisha hivyo kutokana na miundombinu itakayojengwa kwenye eneo hilo, itawawezesha kupiga hatua kubwa kwa haraka na kumfanya Mhe. Rais kujivunia kuwapatia eneo hilo.

 

Naye Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mji Mhe. Ally Makoa amesema mapendekezo ya ya kupatiwa eneo waliloomba kutoka kwenye mpaka wa Magereza waliyowasilisha kwa Rais, ndicho kilichoamuliwa hivyo wananchi hao wataendelea kutumia eneo lao la mashamba huku Magereza nao wakibaki na eneo lao. Hakusita kutoa pongezi zake kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta wataalamu kutoka Wizarani kwa ajili ya kujenga miundombinu kwenye eneo hilo pamoja na kuridhia mapendekezo ya wananchi.

 

MAKAMU WA RAIs AFANYA MAZUNGUMZO NA WAANDISHI WA KITABU CHA UONGOZI WA RAIS SAMIA




 

Monday, January 23, 2023

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI KILICHOFANYIKA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.





 

SIASA ZA KIISTARABU ZA RAISI SAMIA NA KUMBUKUMBU YA TUKIO LA " DINNER TABLE BARGAIN 1790 " NCHINI MAREKANI

Ilikuwa Usiku Wa June 20, 1790 Wakati Mikutano Ya " Congress " Inafanyika Jijini Newyork .Thomas Jefferson Wakati Huo Akiwa Secretary Of The State( Baadae Raisi Wa Tatu Wa Marekani) Alipoamua Kuwaalika Chakula Cha Usiku Watu Wawili Alexander Hamilton Wakati Huo Akiwa Secretary Of Treasure  Na James Madison Mwakilishi Wa Jimbo La Virginia( Baadae Raisi Wa Nne Wa Marekani).

Ni Majadiliani Katika Kikao Hiki "Dinner Table Bargain Of 1790" Kilichoitishwa Na Jafferson Ndicho Kilicholeta Suluhu Hasa Baada Ya Madison Kukubali Hoja Ya Hamilton Na Kushawishi Majimbo Ya Kusini Kuunga Mkono Hoja Na Kwa Pamoja Kulijenga Taifa Lao Ambalo Leo Ni Moja Ya Mataifa Makubwa Na Yenye Nguvu Duniani.


Na Kassim Mpingi  Rufiji-Pwani 

Bila Shaka Taifa Linaunganishwa Na Siasa Za Umoja,Mshikamano,Kusameheana Na Kujenga Nchi Kwa Pamoja(4R).

Vyama Pinzani Baada Miaka Saba Vinaingia Tena Mtaani Kufanya Mikutano Na Kufurahi Matunda Ya Siasa  Safi Na Za Kiistarabu Za Raisi Samia .

Aina Hii Ya Siasa  Anayofanya Raisi Samia Imenifanya Nikumbuke Tukio Muhimu Katika Historia Ya Siasa Za Kiistarabu Duniani Lililotokea Nchini Marekani Mwaka 1790  Lijulikanalo Kama " Dinner Table Bargain " Au " Great Compromise Of 1790 "

Ilikuwa Usiku Wa June 20, 1790 Wakati Mikutano Ya " Congress " Inafanyika Jijini Newyork .Thomas Jefferson Wakati Huo Akiwa Secretary Of The State( Baadae Raisi Wa Tatu Wa Marekani) Alipoamua Kuwaalika Chakula Cha Usiku Watu Wawili Alexander Hamilton Wakati Huo Akiwa Secretary Of Treasure  Na James Madison Mwakilishi Wa Jimbo La Virginia( Baadae Raisi Wa Nne Wa Marekani).

Mualiko Huu Ulisukumwa Na Tofauti Kubwa Na Uhasama Uliokuwa Wakati Huo Katika Ujenzi Wa Taifa  La Marekani .

Tofauti Kubwa Iliyopelekea Kugawanyika Kwa Taifa Lao Ni Hoja Ya Hamilton Na Wenzake Kuwa Serikali Ya Shirikisho (F.G) Ibebe Madeni Ya Majimbo Yatokanayo Na Vita Vya Mapinduzi .Hoja Hii Ililigawa "Congress"  Majimbo Ya Kaskani Yaliunga Mkono Hoja Hii Kwa Vile Madeni Yao Yalikuwa Ni Makubwa Na Wasingeweza Kuyalipa  Huku Majimbo Ya Kusini Akiwemo Madison Wakipinga Kwa Kuwa Wao Walishalipa Madeni Yao.

Na Hoja Ya Pili Ilikuwa Wapi Yawe Makao Makuu Ya Taifa Lao La Marekani .

Ni Majadiliani Katika Kikao Hiki "Dinner Table Bargain Of 1790" Kilichoitishwa Na Jafferson Ndicho Kilicholeta Suluhu Hasa Baada Ya Madison Kukubali Hoja Ya Hamilton Na Kushawishi Majimbo Ya Kusini Kuunga Mkono Hoja Na Kwa Pamoja Kulijenga Taifa Lao Ambalo Leo Ni Moja Ya Mataifa Makubwa Na Yenye Nguvu Duniani.

Na Ni Katika Kikao Hii Ndio Maamuzi Ya Kuwa Makao Makuu Ya Taifa Lao Kuwa Newyork Yalifikiwa

Ndio Maana Tunasema Wakati Huu Nchi Inaunganishwa Na Siasa Za Kiistarabu Za Samia Kupitia Sera Yake Ya "4R" Ni Vyema Kukumbuka Moja Ya Tukio Muhimu Katika Historia Ya Siasa Za Kiistarabu Ulimwenguni.

" The Great Compromise of 1790 

Saturday, January 21, 2023

Monday, January 9, 2023

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amuapisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na Ndugu Griffin Venance Mwakapeje, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya Hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu Griffin Venance Mwakapeje na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Katibu wa Tume ya kurekebisha Sheria Ndugu Griffin Venance Mwakapeje na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.

 

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Natu El-Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.


 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya Hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.




Tuesday, January 3, 2023

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ATANGAZA KURUHUSU KUFANYIKA KWA MIKUTANO YA HADHARA KWA VYAMA VYA SIASA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Vyama Vya Siasa kuhusiana na maamuzi ya Serikali ya kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya Hadhara kwa Vyama hivyo wakati wa Kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.

 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Vyama Vya Siasa kuhusiana na maamuzi ya Serikali ya kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya Hadhara kwa Vyama hivyo wakati wa Kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.

 


Sehemu ya Viongozi mbalimbali wa Vyama Vya Siasa 19 waliohudhuria Kikao kilichoitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.

 






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya Kikao na Viongozi wa Vyama vya Siasa Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene, Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis Mutungi, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Mohammed Ally Ahmed pamoja na viongozi wa Vyama Vya Siasa mara baada ya Kikao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.