Matokeo chanyA+ online




Tuesday, April 18, 2023

JK AKUTANA NA WANARIADHA GABRIEL GEAY NA WENCE TARIMO MJINI BOSTON, MAREKANI

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wanariadha Gabriel Geay (kushoto kwake) na Wence Tarimo (kulia kwake) ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar na kushoto ni mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo.


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya jezi toka kwa mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo wakati alipoonana na wanariadha Gabriel Geay (kushoto kwake) na Wence Tarimo (kulia kwake) ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar.



Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha mwanariadha Gabriel Geay mjini Boston Marekani, siku moja baada ya shujaa huyo kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon.


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kitabu mwanariadha Gabriel Geay mjini Boston Marekani, siku moja baada ya shujaa huyo kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon.



Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wanariadha Gabriel Geay (kushoto kwake) na Wence Tarimo (kulia kwake) ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar.


Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  na Mhe. Saada Mkuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Fedha na Uchumi - wa Zanzibar wakiwa na Watanzania waishio Marekani pamoja na wanariadha Gabriel Geay  na Wence Tarimo ambao walishiriki katika Mashindano ya Riadha yaliyofanyika Boston, Marekani tarehe 17 Aprili 2023, ambapo Geay aliibuka mshindi wa pili. Kulia ni mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo na kushoto ni mtoto wa Bongo Zozo.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  mhamasishaji mashuhuri Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo aliyeongozana na  mwanariadha Gabriel Geay alipokutana nao mjini Boston Marekani, siku moja baada ya shujaa huyo kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon.





 

KAMATI KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA DIPLOMASIA YA UCHUMI YAANZA KAZI RASMI

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Kamati ya Kutathmini Utendaji wa Wizara alipokutana nayo jijini Dodoma tarehe 18 Aprili 2023 kama ishara ya kuanza rasmi kwa kazi ya Kamati hiyo. Kamati hiyo ambayo iliundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 28 Machi, 2023 inao wajumbe saba (7) na inaongozwa na Balozi Msatafu, Mhe. Hassan Simba Yahya (wa kwanza kushoto)
Kikao na Kamati kikiendelea
Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianio wa Afrika Mashariki, Balozi Mstaafu, Mhe. Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax
Mjumbe wa Kamati, Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar akiwa kwenye Kikao kati ya Kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax. Kushoto ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati hiyo
Wajumbe wengine wa Kamati ambao ni Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (kulia) na Balozi Peter Kalaghe wakati wa kikao kati ya kamati hiyo na Mhe. Dkt. Tax

Mjumbe wa Kamati, Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka (kulia) akiwa na Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati (kushoto)
Wajumbe wengine wa Kamati ambao ni Balozi Tuvako Manongi (kushoto) na Mhe. Balozi George Madafa wakati wa kikao kati ya Kamati na Mhe. Waziri Tax
Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati wakifuatilia kikao

Kikao kikiendelea

Mhe. Dkt. Tax (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Kamati Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Simba (wa pili kushoto mstari wa kwanza) pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo

Mhe. Dkt. Tax (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja  na Mwenyekiti wa Kamati ya Kutathmini utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Simba (wa pili kushoto mstari wa kwanza), Wajumbe wa Kamati pamoja na Sekretarieti ya Kamati hiyo


Tuesday, April 11, 2023

WAMILIKI WA ARDHI NCHINI KUANZA KUPOKEA BILI ZA KODI YA ARDHI KUPITIA SIMU YA MKONONI


 








                                

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema wamiliki wa ardhi nchini hivi karibu wataanza kupokea bili za kodi ya pango la ardhi kupitia simu ya mkononi.

 

Dkt Mabula amesema hayo leo tarehe 11 April 2023 wakati Makamu wa Rais Dkt philip Isdori Mpango aliposimama kwa muda kuzungumza na wananchi wa Hungumalwa wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakati wa mwanzo wa ziara yake ya siku tatu mkoani humo.

 

"Ninapozungumza sasa mikoa kumi tayari imeunganishwa katika mfumo na tutaanza kupata bili zetu kupitia simu ya mkononi hivi karibuni maana watu walikuwa wakihoji kama maji waliweza kwanini ardhi wasiweze". Alisema Waziri Mabula.

 

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa sasa kuna wataalamu  26 wanaboresha mifumo ndani ya wizara hiyo lengo likiwa kuhakikisha mifumo ya wizara inaimarika katika masuala ya malipo ili kuwawezesha miliki wa ardhi kuondokana na changamoto za ulipaji kodi ya pango la ardhi.

 

" Napenda niwahakikishie wanannchi wa Hungumalwa, Kwimba na wana Mwanza kwa ujumla kuwa zile kelele za ardhi zinaenda kuisha kwa sababu mama Samia ameiwezesha wizara" alisema Dkt Mabula.

 

Aidha, amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua nchi na kuhitaji kuwa na wawekezaji na kubainisha kuwa wawekezaji lazima wakute ardhi zipo na zimepangwa na kuwekwa kwa uwekezaji.

 

"Niwaombe katika kutenga maeneo ya uwekezaji lazima tuhakikishe yametambuliwa na yanamilikiwa lengo muwekezaji akija asianze kuvutana na wananchi, halmashauri na serikali ya kijiji husika  iwe imefanya utaratibu wa kulitambua eneo na kumiliki" alisema Dkt Mabula.

 

Wednesday, March 29, 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimpokea Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam tarehe 29 Machi 2023 kuanza ziara nchini Tanzania






 

Rais Mhe. Samia akutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Katoliki la Marekani (Catholic Relief Services) Bw. Sean Callahan Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Katoliki la Marekani (Catholic Relief Services)  Bw. Sean Callahan aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Katoliki la Marekani (Catholic Relief Services)   Bw. Sean Callahan pamoja na Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania TEC Padri Charles Kitima mara baada ya mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Katoliki la Marekani (Catholic Relief Services)   Bw. Sean Callahan pamoja na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam