Matokeo chanyA+ online




Saturday, December 9, 2023

NCHI WANACHAMA WA EAC ZAHIMIZWA KUWAUNGA MKONO WAJASIRIAMALI KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA AJIRA


Makamu wa Rais wa Burundi, Mhe. Prosper Bazombaza akitoa hotuba tarehe 08 Desemba 2023 wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Bujumbura tarehe 08 Desemba 2023. Maonesho hayo ambayo yamewashirikisha wajasiriamali zaidi ya 1,000 kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanafanyika kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023.

Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali wadodgo na wa kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo yanayofanyika jijini Bujumbura, Burundi kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023
Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa akishiriki  hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati yanayofanyika jijini Bujumbura
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati yanayofanyika jijini Bujumbura

Makamu wa Rais wa Burundi, Mhe. Prosper Bazombaza  akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Tanzania mara baada ya kufungua rasmi Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika ijini Bujumbur. Wanaoshuhudia ni Mhandisi Luhemeja (kushoto) na Mhe. Balozi Byakanwa

Makamu wa Rais wa Burundi, Mhe. Prosper Bazombaza akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Mhandisi Luhemeja, Mhe. Balozi Byakanwa na wageni wengine walioshiriki ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mhe. Mhandisi Luhemeja akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Afrika Mashariki,  Bw. Josephat Rweyemamu alipotembelea Banda la Tanzania    





Sunday, December 3, 2023

 Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi Kaskazini mwa Tanzania na hali mbaya inayokumba sehemu ya Kaskazini mwa Tanzania, hasa karibu na mteremko wa Mlima Hanang, ambapo mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yametokea. Kulingana na maafisa wa eneo, hadi sasa, watu 47 wamepoteza maisha na wengine 80 wamejeruhiwa kutokana na janga hili.



Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa familia zilizoathiriwa na tukio hili kupitia kipande cha video kilichotumwa wakati wa Mkutano wa Mara kwa Mara (COP 28) huko Dubai, Falme za Kiarabu. Rais Samia amepeleka vikosi vya usalama vya kitaifa kusaidia juhudi za uokoaji na kuzuia maafa zaidi.

Nyumba nyingi na miundombinu imeharibiwa kutokana na hali mbaya ya hewa. Mafuriko yamekuwa tishio kubwa nchini Tanzania, na tukio hili linakumbusha umuhimu wa jitihada za pamoja za kuzuia na kukabiliana na majanga ya asilia. Mkoa wa Manyara umekuwa miongoni mwa maeneo yanayokumbwa na mafuriko mara kwa mara.


Afrika Mashariki imeathiriwa sana na mafuriko na maporomoko ya ardhi mwaka 2023, hali inayochangiwa kwa sehemu na hali ya hewa ya El Niño. Mwezi uliopita, maeneo mbalimbali nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, Kigoma, Kagera, Geita, na Unguja, yalikumbwa na mafuriko na uharibifu wa mali kufuatia mvua kubwa.

Wakulima wameathirika vibaya, na mazao yao yamechukuliwa na maji, hivyo kuathiri maisha yao. Shirika la utabiri wa hali ya hewa nchini Tanzania linaonya kuwa mvua itaendelea kunyesha mwezi huu, na hivyo kuzidi kuongeza hatari ya mafuriko na maporomoko ya ardhi.


Tunatoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya serikali na mamlaka husika. Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuchangia kwa njia yoyote ile ili kusaidia waathirika na kuzuia madhara zaidi. Serikali inaendelea kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu hali ya dharura na hatua zinazochukuliwa.
Tunatoa pole kwa familia zilizoathiriwa na tunaungana na Rais Samia Hassan katika kuwapa moyo waathirika wa janga hili. Tuendelee kusaidiana na kusimama pamoja katika kipindi hiki kigumu.
 

TAMASHA LA FAMILIA YA VIZIWI DUNIANI 2024 KUFANYIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI










Wednesday, November 22, 2023

Hakutakuwa na watoto watakao tembea umbali mrefu kufuata elimu

Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inajenga shule mpya nchini ili kutatua changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata elimu na kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani.

Dkt. Msonde amesema hayo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Mputa inayojengwa kupitia fedha za mradi wa SEQUIP Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

“Serikali haijengi shule kwasababu ya kujifurahisha au kumridhisha mtu bali inajenga shule kwa lengo la kuwawezesha watoto wasitembee umbali mrefu kufuata elimu, lengo la Mhe. Rais kujenga shule ni kuwawezesha watoto wa kitanzania wanaoingia sekondari kumaliza masomo bila kisingizio cha umbali ili waondoke na ujuzi na umahiri wa kujiletea maendeleo yao pamoja na kuleta maendeleo ya jamii zao na taifa kwa ujumla,” amesema.

Ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwa kuchagua eneo zuri la kujenga Shule ya Sekondari ya Mputa na kuongeza kuwa, ujenzi wake ukikamilika vizuri inaweza kuongezwa hadhi ya kuwa na kidato cha tano na cha sita.

Awali, akitoa taarifa ya ujenzi huo, Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari Mputa, Godlove Chumi amesema ujenzi umefikia asilimia 71 na hadi sasa Sh.Milioni 379.9 zimetumika kati ya Sh.milioni 560.5 zilizopelekwa kupitia mradi wa SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya.

:Tamisemi

Saturday, November 18, 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa wito wa kulinda na kuhifadhi mazingira ya Ziwa Tanganyika na rasilimali zake.


Ziwa Tanganyika ni moja ya maziwa makubwa ya Afrika ya Kati likienea mpakani mwa Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Zambia.

Ni ziwa kubwa la pili duniani kwa wingi wa maji matamu baada ya Ziwa Baikal (Siberia) kwa kuzingatia kiasi cha maji ndani yake na kina (hadi mita 1,470).

Kwa kulinganisha eneo lake (km² 32,893) ni la pili tu baada ya Viktoria Nyanza katika Afrika.

Maji yake hutoka kuelekea mto Kongo ha hatimaye katika Bahari Atlantiki.






Dkt. Jafo alitoa wito huo wakati wa Mkutano wa 11 wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika uliofanyika Zambia. Alisisitiza kuwa ziwa hilo ni zaidi ya kapu la chakula na nyumbani kwa watu milioni 13, na hivyo ni jukumu letu kulinda rasilimali zake.

Mkutano huo ulitumika kutoa mwongozo kuelekea matumizi endelevu ya rasilimali za ziwa na kushuhudia tukio la kutia saini Itifaki ya Maendeleo ya Ufugaji wa Majini katika Ziwa Tanganyika na bonde lake. Dkt. Jafo pia alishukuru wadau wa maendeleo kwa juhudi zao katika usimamizi endelevu wa ziwa hilo.

Katika kufunga mkutano, Dkt. Jafo alimpongeza Mhe. Mhandisi Dkt. Collins Nzovu wa Zambia kwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza Kuu la Mawaziri. Mkutano ulijadili masuala muhimu kama vile uwezekano wa kuwajumuisha Makatibu Wakuu katika Vyombo vya Sheria vya LTA, Itifaki ya Maendeleo ya Kilimo cha Majini kwa Ziwa Tanganyika, utafiti wa bioanuwai, na hali ya utekelezaji wa miradi mbalimbali. Washiriki walipokea pia taarifa kuhusu michango ya kitaifa na mpango wa kazi wa mwaka pamoja na bajeti ya LTA ya mwaka 2024.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi nne wanachama wa ziwa hilo, na ujumbe wa Tanzania uliokuwa na Naibu Katibu Mkuu (Muungano), Mkurugenzi wa Mazingira, na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikagua Gwaride la Heshima kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Kundi la 04/20-Shahada ya Sayansi ya Kijeshi.








Wednesday, November 15, 2023

BWAWA LA NYERERE NI ZIWA JIPYA ULIMWENGUNI



Linakuwa Eneo la tisa kwa ukubwa Ulimwenguni, la nne kwa ukubwa barani Afrika, na kubwa zaidi Mashariki mwa Afrika. Kwa urefu wa kilomita 100 (maili 62), upana wa kilomita za mraba 1,200 (maili za mraba 460), Likizuiwa naukuta wa konkriti wenye urefu wa mita 134 [futi 440] likiwa na kiasi cha maji cha mita za ujazo bilioni 34. linakuwa ziwa jipya kuzalishwa  ulimwenguni  hiki cha kuzalisha umeme, Julius Nyerere Hydropower Station. Bwawa la Mteremko wa Stiegler,..Sisi ni Tanzania..na haya ndio matokeochanya+