Matokeo chanyA+ online




Thursday, June 15, 2017

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA KAMPUNI YA BARRICK GOLD CORPORATION IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JUNE 14,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thorntonalipofika Ikulu kwa Mazungumzo, kulia ni Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles June 14, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Prof. John L. Thornton alipofika Ikulu kwa Mazungumzo June 14, 2017 

Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton wakiongea na waandishi wa habari mara baada ya Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu June 14, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  Mwenyekiti wa Barrick  Gold Corporation  Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam  Juni 14, 2017. wakiwa na  Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na  Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton pamoja na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiagana Mhe. Ian Myles balozi wa Canada Nchini pamoja na  Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton alipofoika ikulu kwa mazungumzo juni 14,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi  baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa  Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton  Ikulu jijini Dar es salaam  Juni 14, 2017.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA KAMATI YA PILI YA UCHUNGUZI WA MADINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JUNE 12,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini wakati ikifunguliwa kwenye kabrasha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumkabidhi Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hiyo ya Kamati ya Pili ya Uchunguzi wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Spika wa Bunge Job Ndugai, Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi, Mwenyekiti wa kamati ya pili ya Madini Propfesa Nehemiah Osoro pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo waliojumuika na viongozi wa Dini Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali wakifatilia kwa makini Ripoti ya pili ya Kamati ya Madini Ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS ASISITIZA MAKUBALIANO YENYE FAIDA KWA TAIFA

TUNAMUUNGA MKONO RAIS WETU

WITO WATOLEWA JUU YA WAWEKEZAJI MATAPELI

SERIKALI YA TANZANIA YAWATAKA WANANCHI KUTOA MAONI YA MAREKEBISHO YA SHE...

WAZUNGU WAKILI KUFANYA HUJUMA ZA RASILIMALI ZA NCHI ZA DOMINICA NA SAUDIA

MZUNGU WA BARRICK AKUTANA NA RAIS MAGUFULI

NI LAZIMA TUPATE HAKI YETU RAIS MAGUFULI AONYESHA MSIMAMO

Sunday, June 11, 2017

MATUKIO:PICHA MBALIMBALI UWASILISHWAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/2018

Waziri wa Fedha na Mpango Mhe. Dr. Philip Mpango akiwaonyesha waandishi wa Habari mkoba wenye hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th June 2018.
 Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18.
 Wabunge wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th Juni 2018.
 Baadhi ya wageni wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th Juni 2018.
 .Wabunge wakiingia Ukumbi wa Bunge kusikiliza hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th June 2018.

Picha zote na MAELEZO, DODOMA.

Saturday, June 10, 2017

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) IMETOA GAWIWO LA SHILINGI BILIONI 1.7 KWA SERIKALI


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Sam Kamanga, akizungumza jambo wakati wa tukio la Shirika hilo kukabidhi gawiwo kwa Serikali, kiasi cha Sh. Bil. 1.7, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, katika hafla ya makabidhiano ya gawiwo la Sh. Bil.1.7 liyofanyika mjini Dodoma.
Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakishiriki tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kufanya vizuri kibiashara katika Mwaka wa Fedha 2016/2017, tukio lililofanyika makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, mjini Dodom
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika, akifurahia jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kupata faida katika mwaka wa fedha 2016/2017
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akisisitiza jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kukabidhi Serikalini gawiwo la Sh. bil. 1.7, baada ya Shirika hilo kupata faida kibiashara katika mwaka wa Fedha 2016/2017, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akitoa neno la Shukrani kwa uongozi Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa ubunifu na uwajibikaji wao ulioliwezesha Shirika hilo kupata faida na kutoa gawiwo kwa Serikali, Mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)