Matokeo chanyA+ online




Friday, October 23, 2020

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA ARUSHA MJINI




Sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba ya Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiwaomba kura katika mkutano wa Kampeni za Urais uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo tarehe 23 Oktoba 2020




Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Arusha katika mkutano wa Kampeni za Urais uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo tarehe 23 Oktoba 2020








Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Arusha katika mkutano wa Kampeni za Urais uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo tarehe 23 Oktoba 2020

LETENI MBUNGE WA KUPITISHA BAJETI, SIYO WA KUPINGA TU - KASSIM MAJALIWA

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Kilwa wamchague mbunge ambaye atakuwa tayari kupitisha bajeti na kuwaletea maendeleo.

“Msilete watu wa kukataa fedha, bali leteni mtu wa kukubali fedha zipitishwe ili mpate maendeleo,” amesema.

Ametoa wito huo  (Alhamisi, Oktoba 22, 2020) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa Ilulu Njianne katika kata ya Tingi na kata ya Kivinje kwenye mikutano iliyofanyika wilayani Kilwa, mkoani Lindi.

“Tanzania inahitaji watu makini na pale Bungeni siyo mahali pa viburudisho. Bunge linahitaji watu wa kuwasemea wananchi na siyo kuleta burudani wakati wengine wako kazini,” amesema.

Mheshimiwa Majaliwa leo yuko mkoani Lindi kumuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli. Ametumia fursa hiyo kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo ya Kilwa Kaskazini, Bw. Francis Ndulane na Kilwa Kusini, Bw. Ally Kasinge pamoja na wagombea udiwani wa kata za majimbo hayo kwa tiketi ya CCM.

“Mleteni mtu anayeweza kujenga hoja na kuitetea. Fedha zisipopitishwa maendeleo yenu hayawezi kuja kwa sababu hakuna mtu wa kuwasemea. Wana-Kilwa msiniangushe, Jumatano ijayo ikifika, chukua karatasi yako weka tiki kwa Dkt. Magufuli; kwa mbunge wa CCM na kwa diwani wa CCM.”

Aliwataka wakazi hao wawachague wagombea wa CCM kwa sababu chama hicho kina makada wazuri na kimewaandaa vizuri viongozi wake. “Kitendo cha Kamati Kuu kuwapa nafasi hawa waliopitishwa, hakikuwa na nia ya kumuonea mtu bali kuwapanga viongozi wake kulingana na majukumu.”

Mapema, mtia nia aliyeongoza kwenye kura za maoni katika jimbo la Kilwa Kaskazini, Bw. Murtaza Mangungu alipopewa nafasi ya kuwaombea kura wagombea wa CCM alitumia fursa hiyo kuwaonya watu wanaoweka maneno maneno dhidi yake.

“Wako watu ambao walitaka kusafiria nyota yangu. Wakati tunazindua kampeni, nilitamka kutoka moyoni mwangu, siyo kinywani tu, kwamba nitafanya kazi kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinashinda. Namuombea kura Dkt. Magufuli, namuombea kura kaka yangu Francis Ndulane na mgombea udiwani wa Tingi, Rajab Ngatanda,” alisema.

Thursday, October 22, 2020

MWAMBE, KATANI WAELEZA MACHUNGU YA UPINZANI


Wagombea Ubunge wawili wa Mkoa wa Mtwara waliotoka vyama vya upinzani na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) wameeleza machungu waliyokuwa wakikumbana nayo wakati wakitaka kuwatumikia wananchi wao. 

 

Wabunge hao Bw. Cecil Mwambe (Ndanda) na Bw. Katani Ahmed Katani (Tandahimba) ambao wamehamia CCM kwenye kinyang’anyiro hiki cha ubunge, wamewaonya wakazi wa Masasi wasifanye makosa ya kuchagua wagombea wa upinzani kwani wataendelea kukosa maendeleo.

 

Wametoa wito huo jana (Jumatano, Oktoba 21, 2020) kwenye mkutano wa kuwanadi wagombea ubunge na udiwani wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba kata ya Mkuti, wilayani Masasi, mkoani Mtwara ambako Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi.

 

Bw. Mwambe anayegombea Ndanda na ambaye alihamia CCM akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema licha ya kuwa alikuwa akitamani wananchi wake wapate huduma muhimu kama maji, afya na barabara, haikuwa rahisi kwake kuchangia bajeti ya maendeleo kwa sababu walikuwa wanakatazwa.

 

“Mambo yaliyokuwa yanafanyika huku Masasi hata sisi kule Ndanda tulikuwa tunayatamani. Hii ni kwa sababu hakuna cha maana kule kilichoandikwa kwa ajili yenu, na mimi ni shahidi. Katika miaka mitano ya ubunge wangu, sijawahi kuitikia NDIYO na madhara yake nimeyaona. Ninawaomba sana, msifanye makosa hayo,” alisema.


Naye Bw. Katani anayegombea Tandahimba na ambaye alihamia CCM akitokea Chama cha Wananchi (CUF), aliwataka wananchi hao wasifanye makosa kwa sababu kule alikokuwa hawana ilani.


“Kama Katani anayeongea hapa mbele yenu, alikuwa Mwenyekiti wa Vijana Taifa na kaikimbia CUF, wewe ni nani mwananchi wa Masasi hata upinge maendeleo ya nchi hii? Tena niwaambie, kule hakuna ilani. Nawaomba wana Masasi msifanye makosa ya kuchagua wagombea wa upinzani, sisi wenzenu tumeyaona tukiwa Bungeni.”


“Ukienda Bungeni kutaka kusema Masasi tuna shida ya umeme, wakubwa wanasema kapinge bajeti. Tutaupataje umeme? Tumekwenda Bungeni tumepiga plasta, sasa ukitaka kuomba umeme, utaongea vipi na wewe midomo umeifunga plasta?”


“Wana Masasi msitucheleweshe, hii gari ya Dkt. Magufuli inatelemka kwa kasi kuleta maendeleo huku mikoa ya Kusini. Acheni Geofrey Mwambe awe mbunge wa jimbo la Masasi, alete maendeleo,” alisisitiza.


Wakati huohuo, mwanasiasa mkongwe na Waziri Mstaafu, Mama Anna Abdallah alisema anashangazwa na tabia ya mgombea urais ambaye anatangaza kwamba ndoa za jinsia moja ni haki ya msingi ya wananchi.


“Yuko mgombea wa urais ambaye yeye anasema haonei aibu ushoga eti anauunga mkono. Yaani mwanaume amuoe mwanaume mwenzake na mwanamke amuoe mwanamke mwenzake.”


“Anasema eti ni haki za binadamu. Hivi kama baba yake angemuoa mwanaume mwenzake au mama yake angeolewa na mwanamke mwenzake, yeye leo angekuwepo na angekuja kugombea urais?”


“Rais wa namna hiyo ana mawazo ya kishetani, hakuna dini hata moja inayosema juu ya ushoga. Hata wanaogombea kwa kupitia chama hicho ninaanza kuwatilia shaka. Hakuna ushoga katika nchi hii, hatutakiii! Haiwezekani, sisi tulioko hapa tumezaliwa na sisi tumezaa. Watoto wetu waache kuzaa kwa ajili ya mtu mmoja anayesema hiyo ndiyo haki. Hakuna haki kwenye ushoga, ni dhambi,” alisisitiza.


Mapema, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Masasi, Bw. Rashid Chuachua alisema katika wilaya hiyo, ndani ya miaka mitano, waliwezaa kujenga madarasa 108 ya shule za sekondari na mengine 355 ya shule za misngi.


Alisema kiasi cha sh. bilioni 3.5 kilitolewa kwa ajili ya elimumsingi bila malipo huku sekta ya afya ikiboreshwa kwa kujenga kituo cha afya cha Mbonde kwa gharama ya sh. milioni 500 na hospitali ya Mkomaindo ikipatiwa jengo la upasuaji lililogharimu sh. milioni 228.


“Mradi wa maji unaendelea kujengwa na ukikamilika, hatutakuwa na shida kabisa ya maji hapa Masasi,” alisema na kuwaombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Masasi, Bw. Geofrey Mwambe; na wagombea udiwani 14 wa CCM wa jimbo la Masasi.

 

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA HAI MKOANI KILIMANJARO

 Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wananchi wa Hai mara baada ya kuwasili Bomang’ombe Hai mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni za CCM leo tarehe 22 Oktoba 2020.

 





Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Hai mkoani Kilimanjaro katika mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika Bomang’ombe leo tarehe 22 Oktoba 2020.

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wananchi wa Hai mara baada ya kuwasili Bomang’ombe Hai mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni za CCM leo tarehe 22 Oktoba 2020.

Wednesday, October 21, 2020

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO






 Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Moshi waliofurika katika mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro leo tarehe 21 Oktoba 2020.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Rais Dkt John Magufuli akimvua Kofia ya Chama Cha TLP na Kumvisha Kofia ya Chama Cha Mapinduzi-CCM Mwenyekiti wa Chama Cha TLP Augustine Lyayonga Mrema eneo la himo akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano wa Kampeni Moshi Mjini
 

 

Sehemu ya Wananchi wa Moshi waliohudhuria Mkutano wa Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli uliofanyika katika uwanja wa Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro leo tarehe 21 Oktoba 2020.


Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mkutano wa Kampeni za CCM leo tarehe 21 Oktoba 2020.
 

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Himo katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuwasili wakati akitokea Same mkoani Kilimanjaro leo tarehe 21 Oktoba 2020. 
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustine Mrema mara baada ya kuwasili Himo mkoani Kilimanjaro leo tarehe 21 Oktoba 2020.

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Beberu la Mbuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha TLP Augustine Mrema mara baada ya kuwasili Himo mkoani Kilimanjaro leo tarehe 21 Oktoba 2020.




Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya mara baada ya kuwasili Mwanga mkoani Kilimanjaro leo tarehe 21 Oktoba 2020.


Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amemshika mkono Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Vunjo Charles Kimei mara baada ya kumuombea Kura kwa wananchi wa Himo.