Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kulia) akisaini kitabu cha mahudhurio ya Wageni alipotembelea banda la maonesho la Wizara ya Mifugo na Uvuvi yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma. Maonesho hayo yalikuwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni Juni 5, 2022. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Sekta ya Uvuvi, Bw. Melton Kalinga. Wengine kushoto ni Maafisa, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Sekta ya Uvuvi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) akipatiwa maelezo kuhusu uandaaji na uhifadhi wa malisho ya mifugo na Afisa Mifugo Mkuu, Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (Sekta ya Mifugo), Bw. Deograsias Ruzangi alipotembelea banda la maonesho la Wizara ya Mifugo na Uvuvi yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.