Matokeo chanyA+ online




Monday, March 6, 2023

MAKAMU WA RAIS MAZUNGUMZO NA GREEN CLIMATE FUND

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi - Uwezeshaji Sekta Binafsi wa Green Climate Fund Bw. Soji Omisore, Mazungumzo yaliofanyika Doha nchini Qatar  tarehe 06 Machi 2023.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Msaidizi - Uwezeshaji Sekta Binafsi wa Green Climate Fund Bw. Soji Omisore mara baada ya Mazungumzo baina yao yaliofanyika Doha nchini Qatar  tarehe 06 Machi 2023.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na  Mkurugenzi Msaidizi - Uwezeshaji Sekta Binafsi wa Green Climate Fund Bw. Soji Omisore na Meneja wa kanda ya Asia – Pacific wa Green Climate Fund Bi. Anupa Lamichahane mara baada ya Mazungumzo baina yao yaliofanyika Doha nchini Qatar leo tarehe 06 Machi 2023. Wengine ni Waziri wa Fedha na Mipango  Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Saada Mkuya,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mbarouk N. Mbarouk, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa (New York)  Balozi Dkt. Suleiman H Suleiman pamoja na Msaidizi wa Makamu wa Rais – Mazingira Dkt. Emma Liwenga.



Makamu wa Rais amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Msaidizi - Uwezeshaji Sekta Binafsi wa Green Climate Fund Bwana Soji Omisore, Mazungumzo yaliofanyika Doha nchini Qatar. Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais ametaja athari zinazoikabili Tanzania kutokana na mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame, mafuriko, ongezeko la kina cha bahari ambazo zinapelekea changamoto katika sekta ya kilimo. 

 

Makamu wa Rais amesema Tanzania imeendelea kufanya jitihada mbalimbali katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo inahusisha utengenezaji wa sera kama vile sera ya taifa ya mazingira, mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuandaa mpango kabambe wa mazingira pamoja na usafi na uhifadhi wa mazingira kupitia upandaji miti kila mkoa. Makamu wa Rais ametaja jitihada zingine ambazo ni kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala, kuwekeza katika uhifadhi wa misitu, kuvutia tekenolojia rafiki za mazingira pamoja na mchango wa taifa katika kupunguza gesi joto wa mwaka 2021.

 

Makamu wa Rais amesema Tanzania bado inahitaji kuungwa mkono katika kukabiliana na athari za mbadiliko ya tabia nchi kifedha, kiteknolojia pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu katika kuandaa maandiko ya miradi yenye uwezo wa kupata ufadhili. Pia ametoa wito kwa taasisi ya Green Climate Fund kuiunga mkono Tanzania katika  utoaji elimu ya  biashara ya kaboni na njia nyinginezo za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi - Uwezeshaji Sekta Binafsi wa Green Climate Fund Bwana Soji Omisore amesema taasisi ipo tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi ya uhifadhi wa mazingira. Amesema taasisiya Green Climate Fund itajielekeza pia katika kuwajengea uwezo wa wataalamu wa Tanzania.



 


 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo leo ametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja la Gunyoda, Mbulu ambalo mpaka kukamilika litagharimu shilingi 839,760,000.





 

Tuesday, February 28, 2023

BALOZI SHELUKINDO ASISITIZA UMUHIMU WA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akipokea maua mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023. Balozi Shelukindo aliapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuushika wadhifa huo tarehe 27 Februari 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Fatma Rajab wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Alex Mfungo wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Naimi Aziz wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.


Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Caesar Waitara wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Bw. Japhary Kachenje wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika katika ofisi za Wizara  jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Haji Janabi wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika katika ofisi za Wizara  jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Talha Waziri wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika katika ofisi za Wizara  jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Samwel Shelukindo ajitambulishe kwa menejimenti ya Wizara wakati wa hafla ya mapokezi iliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo (kushoto) akiongoza kikao cha Menejimenti kilichofanyika kwa lengo la kujitambulisha katika ofisi za Wizara jijini Dododma tarehe 28 Februari 2023. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Fatma Rajab. 

Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Alex Mfungo na Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango, Bw. Haji Janabi wakifatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Mkurugenzi Idara ya Afrika, Balozi Naimi Aziz akijitambulisha kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo katika hafla ya mapokezi yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.


Mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caesar Waitara (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Noel Kaganda wakifuatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.

Kutoka kulia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Swalehe Chondoma na Bw. Haji Janabi wakifuatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.


Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Leonce Bilauri na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji wakifuatilia kikao cha utambulisho cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrka Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo.

Sehemu nyingine ya wajumbe wa managementi wakifuatilia kikao.

Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Bw. Amani Mwatonoka na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Salma Baraka wakifuatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dododma tarehe 28 Februari 2023.

Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Dkt. Isaac Kalumu  na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Talha Waziri wakifuatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dododma tarehe 28 Februari 2023.

Mwakilishi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Ally Kondo (Kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Biashara za Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi, Bw., Francis Berege wakifuatilia kikao cha utambulisho wa Katibu Mkuu kilichofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo akiwasili katika ofisi za Wizara  jijini Dodoma tarehe 28 Februari 2023.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo (kulia) akisalimiana na sehemu ya madereva walioshiriki hafla ya mapokezi katika ofisi za Wizara jiji Dodoma tarehe 28 Februari 2023

Picha ya Pamoja






CHANGAMOTO BANDARI YA MALINDI INASABABISHWA NA KUWA NA GATI MOJA DOGO ...

Saturday, February 25, 2023

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Dk. Condoleezza Rice na mfanyabiashara Bill Gates wameungana na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. George W. Bush katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupambana na UKIMWI (President’s Emergency Plan for AIDS Relief - PEPFAR) jijini Washington DC Ijumaa Februari 24, 2023



Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. George W. Bush na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Dk. Condoleezza Rice wakiwa kwenye mjadala katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupambana na UKIMWI (President’s Emergency Plan for AIDS Relief - PEPFAR) jijini Washington DC Februari 24, 2023




Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa 66 wa Mambo ya Nje wa Marekani Dk. Condoleezza Rice katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupambana na UKIMWI (President’s Emergency Plan for AIDS Relief - PEPFAR) katika ukumbi jijini Washington DC Februari 24, 2023


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mfanyabiashara Bill Gates katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupambana na UKIMWI (President’s Emergency Plan for AIDS Relief - PEPFAR) jijini Washington DC Februari 24, 2023


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. George W. Bush katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupambana na UKIMWI (President’s Emergency Plan for AIDS Relief - PEPFAR) jijini Washington DC Februari 24, 2023


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) wa Marekani Bi Alice Albright katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Kupambana na UKIMWI (President’s Emergency Plan for AIDS Relief - PEPFAR) jijini Washington DC Februari 24, 2023


Sherehe hiyo, iliyoandaliwa na Taasisi ya George W. Bush inafanyika  katika Taasisi ya Amani ya Marekani. Watatu hao watashiriki katika mjadala  maalumu utaoendeshwa na Dkt. Rice kuhusu kuanzishwa kwa PEPFAR, mafanikio yake  makubwa, na jinsi programu hiyo inavyofanikiwa katika  nchi washirika na kwa sera ya kigeni za Marekani.


Kwa Mujibu  wa taarifa kutoka Taasisi ya George W. Bush, katika maadhimisho hayo, Mke wa Rais Mstaafu wa Marekani George W. Bush, Bi. Laura Bush, atatoa maelezo mafupi na kuwatambulisha Tatu Msangi na Faith Mang'ehe, Mabalozi wa Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation kutoka Tanzania waliohudhuria wakati wa kutolewa hotuba ya Hali ya Muungano  (State of the Union) katika Congress ya Marekani, kuhusu mpango huo wa PFEPFAR mwaka 2008. 

 

Katika kuadhimisha miaka hiyo 20 ya mafanikio ya PEPFAR, licha ya kwamba Mpango huo unatekelezwa katika nchi mbalimbali Afrika na Asia, Taasisi ya George Bush Foundation wameamua kumualika Dkt. Kikwete kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuufanya Mpango huo kuwa na mafanikio.


Kwa mujibu wa Taasisi ya George W. Bush Foundation, Tanzania imekua ni nchi ya kupigiwa mfano kwa namna ilivyofanya jitihada za kupambana na ugonjwa wa UKIMWI kwa juhudi zake yenyewe kama nchi na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kimataifa kama vile PEPFAR.


Taasisi hiyo inasema kwamba tangu mwaka 2003, PEPFAR imesaidia Tanzania kupunguza vifo vinavyotokana na UKIMWI kwa karibu 80% na maambukizi mapya kwa karibu 60%. Mpango huo ulipoanza, chini ya Watanzania 1,000 walikuwa wakipata matibabu ya VVU. Hivi sasa, zaidi ya Watanzania milioni 1.5 wanapokea matibabu haya ya kuokoa maisha.


Tangu Rais George W. Bush alipozindua PEPFAR mwaka 2003, serikali ya Marekani imewekeza zaidi ya dola bilioni 100 katika mapambano yake ya kimataifa dhidi ya VVU/UKIMWI, zikiwemo karibu dola bilioni 7 kwa Tanzania, ukiwa ni mchango  mkubwa kuwahi kutolewa na taifa lolote kupambana na ugonjwa mmoja katika historia ya binadamu.


 

Friday, February 24, 2023

SEKTA BINAFSI YA TZ KATIKA SHEREHE ZA UFUNGUZI WA JUKWAA LA EUTZBIASHARA LILILOONGOZWA NA MH DKT PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA.








Mbele ya Mh Dkt Philip Mpango, Makamu wa Rais wa #Tanzania, mikataba mitatu yenye thamani ya Euro milioni 353 ilisainiwa kati ya Taasisi za Tanzania na Umoja wa Ulaya.