Matokeo chanyA+ online




Monday, August 14, 2023

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA TAMASHA LA ACCES, WADAU WA MUZIKI ZAIDI YA 1000 DUNIANI KUSHIRIKI

 





Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amefanya kikao na Mkurugenzi wa Taasisi ya “Music in Africa Foundation na ACCES Eddie Hatitye Agosti 14, 2023 jijini Dodoma kuhusu tamasha la ACCES ambalo litafanyika hapa nchini Novemba 9-11, 2023.  

Viongozi hao wamejadiliana namna bora ya kuendesha tamasha hilo kwa kuwashirikisha wasanii wote nchini wakiwemo chipukizi na walifanikiwa katika uga wa muziki.

Lengo la tamasha hilo ambalo linandaliwa na Taasisi ya Music in Africa kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania ni kuwasaidia wanamuziki kutambuana na kuonyesha uwezo wao wa kuimba pamoja nakufundishwa namna ya kuchangamkia fursa za masoko.

Tamasha hilo la ACCES linatarajiwa kuhudhuriwa na wadau wa muziki zaidi ya 1000 kutoka zaidi ya mataifa 50 duniani ambalo kwa Tanzania linafanyika kwa mara ya pili ambapo mwaka jana lilifanyika Novemba 24-26, 2022 jijini Dar es Salaam.


Thursday, August 10, 2023

MKUTANO WA 6 WA UONGOZI WA WANAWAKE WENYE CPA CHINI YA TAWCA UTAFANYIKA JIJINI MWANZA TAREHE16-18 AGOSTI 2023:






















Na Mwandishi wetu

Mkutano wa 6 wa Uongozi wa Wanawake wa TAWCA 2023: kauli mbiu ni "Kuongoza Bila Jina," Kugusa Maisha, Kubadilisha Mtazamo wa Wanawake" Tarehe: 16 - 18 Agosti 2023

Eneo: Malaika Beach Resort, Mwanza, Tanzania

Maelezo Muhimu:

Mkutano wa 6 wa Uongozi wa Wanawake wa TAWCA, ambao utafanyika katika eneo lenye uzuri wa kupendeza la Malaika Beach Resort huko Mwanza, Tanzania. Mkutano huu wenye kaulimbiu ya "Kuongoza Bila Jina", unakusudia kuwahamasisha wanawake kuwa viongozi bila kujali majina yao rasmi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na Kugusa Maisha, Kubadilisha Mtazamo wa Wanawake"


Muhtasari wa Mkutano huo:

  • Hotuba za Motisha na Uongozi kutoka kwa Wasemaji Wenye Uzoefu
  • Majadiliano ya Jopo Kuhusu Uwezeshaji wa Wanawake na Maendeleo ya Uongozi
  • Warsha za Vitendo kuhusu Ujasiri wa Binafsi, Mazungumzo, na Uongozi Bora
  • Fursa za Kujenga Mtandao na Kujifunza Kutoka kwa Wenzako
  • Hafla ya Kufunga yenye Kutoa Mwanga Mpya kwa Maono ya Kesho

Lengo Kuu:

Mkutano huu unalenga kuwawezesha wanawake kuchukua hatua za uongozi bila kujali vyeo vyao, na pia kuwahamasisha kubadilisha mtazamo wao ili kuvunja vizuizi vya ndani na kuleta mabadiliko katika jamii na maisha yao.

Jiunge sasa katika tukio hili la kuvutia la kujenga uongozi, kujifunza kutoka kwa wataalam, na kubadilishana mawazo na wanawake wenzako. Tafadhali jisajili mapema ili kuhakikisha nafasi yako kwenye mkutano huu wa kipekee!


 

Thursday, August 3, 2023

TARI NALIENDELE KIVUTIO MAONESHO YA NANENANE 2023 NGONGO LINDI

Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Naliendele Programu ya Korosho,Kitengo cha Udhibiti wa Visumbufu vya Wadudu waharibifu na Magonjwa, Bobnoel Assenga (kushoto) akitoa maelezo ya Wadudu waharibifu na Magonjwa kwa mkulima Cathbert Richard (kulia) aliyetembelea banda la taasisi hiyo katika Maonesho ya NaneNane 2023 yanayofanyika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. Katikati ni Mtafiti wa Kilimo Bakari Kidunda ambaye pia ni Mratibu wa Uhalishaji Teknolojia na Mahusiano wa taasisi hiyo.

..................................................... 

Dotto Mwaibale na Godwin Myovela, Lindi 

KITUO cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele kilichopo  mkoani Mtwara kimekuwa kivutio kikubwa katika Maonesho ya Nanenane 2023 Kanda ya Kusini yanayofanyika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

Katika Maonesho hayo kituo hicho kinatarajia kuonesha teknolojia za kilimo za kuvutia wakulima kutoka Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi ambao wameombwa kujitokeza kwa wingi kufika katika viwanja hivyo kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kituo hicho Dk. Fortunus Kapinga kuhusu maonesho hayo Mtafiti wa Kilimo Bakari Kidunda ambaye pia ni Mratibu wa Uhalishaji Teknolojia na Mawasiliano alisema wamejipanga vizuri na kuwa wakulima wategemee kupata ujuzi mkubwa wa masuala ya kilimo katika maonesho hayo.

Alisema TARI Naliendele ni miongoni mwa vituo 17 vilivyopo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania ambapo pia wanavituo vingine kama hivyo katika kanda zingine nchini na kueleza kuwa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha teknolojia zinawafikia wakulima.

    Alisema TARI Naliendele wamepewa jukumu la kitaifa la kutafiti zao la korosho, ufuta na karanga na kuwa changamoto zote zinazojitokeza kwenye mazao hayo wao ndio wanaowajibika kutoa majibu.

Kidunda alisema pia wamekuwa wakifanya utafiti wa mazao mengine kwa kushirikiana na vituo vingine vilivyopewa mamlaka kitaifa na kuwa katika maonesho hayo wana programu ya utafiti wa mazao ya nafaka, mikunde, jamii ya mizizi, mbogamboga na matunda.

 Alisema mwaka huu wamejipanga vilivyo kuonesha teknolojia zote za kilimo na litakuwa ni tukio la aina yake kwani kwa wale waliozoea kufika kwenye siku za nanenane sasa wataona shughuli endelevu za kituo hicho na kuwa wamefanya maboresho lukuki ya kisayansi katika kila idara.

" Kituo cha Ngongo sio kwa ajili ya Nanenane tu bali kipo kwa mwaka mzima kueneza teknolojia za kilimo na wataweza kuangalia teknolojia mbalimbali za korosho, mbegu za mafuta, mikungu ya ndizi ya aina Mtwike , jamii ya mikunde na nafaka. Mbali ya hayo pia kutakuwa na shughuli ya kuangalia jinsi ya kuongeza thamani ya zao la korosho, ufuta na zao la karanga ambapo katika zao la korosho watu walizoea kuja na kutafuna korosho lakini sasa watakuja kula na kunywa korosho kwani watakuwa na juisi, jamu na mvinyo zilizotokana na zao hilo" alisema Kidunda.

Alisema katika maonesho hayo watakuwa na kituo chao cha kanda ambacho kitatumika kutoa mafunzo kwa wakulima hivyo wadau mbalimbali wameombwa wafike kwani wataona mengi kwenye zao la korosho, ufuta, karanga, mihogo, viazi vitamu, kunde, choroko, mbaazi, mahindi, uwele na mengineyo.

Alisema mazao yote ambayo yanalimwa kwenye mikoa ya Mtwara, Ruvuma na Lindi na hata yale ambayo hayalimwi katika mikoa hiyo lakini yanaweza kustawi maeneo hayo yatakuwepo katika maonesho hayo.

Kidunda alisema katika kituo chao cha Naliendele wamekuwa hawana msimu pale wameweka teknolojia ambazo zinaonekana kwa mwaka mzima kwa ajili ya wakulima kujifunza hatua mbalimbali za ukuaji wa zao husika kuanzia likiwa kwenye kitalu,  shambani, utumiaji wa viatilifu, udhibiti wa magonjwa na uvunaji wake.

" Tukisema mkulima au mdau aje wakati wa wiki ya Nanenane tu kuna hatua nyingi hawezi kuzielewa na ndio maana tunasema hatufungi maonesho haya tupo kipindi chote cha mwaka mzima." alisema Kidunda.

Alisema TARI imekuwa ikisogeza huduma zake kwa wananchi nchi nzima ili ziwafikie walengwa.

Alisema zamani zao la korosho lilikuwa likilimwa katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani lakini sasa linalimwa karibu mikoa zaidi ya 20 kama Morogoro, Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora, Shinyanga, Katavi, Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe,  Mkoa wa Kilimanjaro na maeneo ya Same.

Alisema kinachosemwa korosho ilimwe wapi sio mipaka ya kiutawala bali ni mahitaji ya kiikolojia.

Kidunda alitumia nafasi hiyo kuwaomba wakulima na wadau mbalimbali kufika kwenye maonesho hayo ya Kanda ya Kusini yanayofanyika Ngongo mkoani Lindi kuanzia Agosti 1,2023 kwenda kujifunza teknolojia za kilimo ambayo yatafikia tamati Agosti 8, 2023.

Kidunda alisema akiwa kama Mratibu wa Uhalishaji Teknolojia na Mahusiano jukumu lake kubwa ni kuhakikisha teknolojia zinawafikia wakulima.

"TARI Naliendele tunafanya utafiti na ukishafanywa kazi yetu ni kutoa matokeo ya utafiti huo na idara yangu kazi yake kubwa ni kuuchambua na kuchakata taarifa za utafiti huo na kuziweka katika lugha nyepesi ambayo inaweza kuwa rahisi kwa wakulima na wadau wengine kuielewa" alisema Kidunda.

Kidunda alisema kauli mbiu ya maonesho hayo mwaka huu ni Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula.

Mtafiti kutoka TARI Naliendele Programu ya Korosho,
Kitengo cha Udhibiti wa Visumbufu vya Wadudu waharibifu na Magonjwa, Bobnoel Assenga alisema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa wakulima
namna ya kudhibiti visumbufu vya wadudu waharibifu na magonjwa, ikiwemo ugonjwa wa Ubwiriunga, ugonjwa wa Blaiti na Debeki ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa ni changamoto kwa ustawi wa zao la korosho ndani ya Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na kwingineko
nchini.

Alisema  Tari Naliendele imekuwa ikikabiliana na kukithiri kwa wadudu waharibifu wa zao hilo wakiwemo Mbu wa Mikorosho, Mbu wa Minazi na Vidung’ata ambao ni kikwazo kikubwa cha ukuaji mzuri wa zao la Korosho ambalo linatajwa kuwa ni zao lenye uchumi mkubwa na soko la uhakika. 

Tuesday, July 25, 2023

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KWA VIONGOZI WANAOSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU RASILIMALI WATU, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 25 JULAI, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu wakati wa hafla ya Chakula cha jioni, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.




Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na wageni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova, Rais wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina pamoja na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Biowakati wakiangalia vikundi mbalimbali vikitumbuiza katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Wonie Bio wakati wa hafla ya chakula cha jioni Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.








Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi pamoja na Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova kabla ya hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.

Wakuu wa nchi mbalimbali pamoja na Viongozi wengine wakiwa kwenye hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya viongozi hao wanaoshiriki Mkutano wa Rasilimali watu Jijini Dar es Salaam Julai 25, 2023.


Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina kabla ya kuelekea kwenye hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu, Ikulu jijini Dar es Salaam .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe tarehe 25 Julai, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa São Tomé na Principe Mhe. Carlos Vila Nova Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2023.


Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa pamoja na viongozi wengine kutoka nchi mbalimbali wakielekea kwenye hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya viongozi wanaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi