Matokeo chanyA+ online




Friday, September 22, 2017

JWTZ LAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI LA UJENZI WA UKUTA MERERANI-SIMANJIRO MKOANI MANYARA

Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ laanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Meja Jenerali Michael Isamuyo atua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano.
Helikopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuyo akitua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano. Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ limenanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
 Helkopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuhyo ikitua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara tayari kwa kukagua eneo litakalojengwa uzio kuzunguka kitalu A hadi D katika eneo la Madini la Tanzanite Mererani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Simanjiro na wananchi mara baada ya kutua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara tayari kwa kukagua eneo litakalojengwa uzio kuzunguka kitalu A hadi D katika eneo la Madini la Tanzanite Mererani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
  Meja Jenerali Michael Isamuhyo akisalimiana na baadhi ya wakazi wa eneo la Mererani,mara baada ya kutua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipenya kwenye vichaka wakati wa kukagua eneo litakalojengwa ukuta.
  Meja Jenerali Michael Isamuhyo akitembelea na kuoneshwa eneo la vitalu A mpaka D katika eneo la machimbo ya Tanzanite Mererani wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 21, 2017, tayari kwa kuanza kazi ya kujenga uzio kuzunguka eneo hilo kufuatia amri ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyotoa jana ili kudhibiti biashara ya madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee. 
 Meja Jenerali Michael Isamuhyo akioneshwa ramani ya vitalu A hadi D katika eneo la madini ya Tanzanite huko Mererani.
Meja Jenerali Michael Isamuhyo akitembelea na kuoneshwa eneo la vitalu A mpaka D katika eneo la machimbo ya Tanzanite Mererani wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 21, 2017, tayari kwa kuanza kazi ya kujenga uzio kuzunguka eneo hilo kufuatia amri ya Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyotoa jana ili kudhibiti biashara ya madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee.

Wednesday, September 6, 2017

RIPOTI MAALUM YA BUNGE KUCHUNGUZA BIASHARA YA TANZANITE NA ALMASI INASIKITISHA

Kwamiaka 12 ya uuzaji madini ya Tanzanite Duniani, yamefikia Trilion 8 huku Tanzania kwa mujibu wa ripoti ndani ya TRA Taifa lilipata Bilion 254 ambapo sawa na 5% tu ya mauzo yote Duniani Repoti inabaini 80% ya Mauzo yote ya Tanzanite yameibiwa Nchini.