PARACHICHI YA NCHI YETU NI URITHI WA ULIMWENGU LINA SOKO KUBWA NCHI ZA ULAYA.
Soko kubwa na bei Nzuri ya
Parachichi imeimarika Nchi za Ulaya za Denmark, Ufaransa, Uholanzi, Norway, Hispania
na Uingereza Likitoa fulsa mpya ya Ustawi wa zao hili kwa Watanzania, imebainika kwamba Parachichi ya Tanzania
imechukua chati ya Ubora katika Soko hilo.
Uchunguzi kitakwimu una baini Mwaka
2012, kiasi cha mauzo ya nje ya Parachichi yalikuwa kilo 488,492 tu, Miaka
mitatu baadae Mwaka 2015 Tanzania ilisafirisha Kilo 2,579,976 Ikiwa ni ongezeko
la 428.48%.
Kwa mujibu wa Kampuni ya Africado
ambayo ni kampuni ya kwanza ya Tanzania
inayosafirisha Parachichi nchini Uingereza ambako maduka makubwa vyakula ya
Ocado, Sainsbury, Tesco na Waitrose, Parachichi ya Tanzania inatajwa kuwa Bora zaidi
katika soko hilo la Ulaya.
Walaji wa Ulaya wamenogewa na
Parachichi linalo zalishwa Mufindi na Kilolo likitajwa kupatikana msimu ambao
Nchi zaidi ya Kumi zinazozalisha Tunda hili kuwa Nje ya Msimu wa Uvunaji wa Zao
hili
Parachichi linazaliswa na Nchi
zaidi ya 10 Duniani zikiwemo Argentina, Brazil, Chile, Colombia, Dominican Republic,
Israel, Kenya, Mexico, Morocco, Peru, South Africa, Spain, Swaziland, Tanzania
Zao la
Parachichi limeonyesha mwenendo mzuri wa bei na Soko kubwa Ulaya likiuzwa kwa
hadi Sh za Kitanzania 7000 ama Paun 1.95 hii leo,fulsa hii inaangukia Tanzania
Kipindi cha mavuno cha sasa ni Juni hadi Agosti, Huku Tanzania pekee
inaweza kuvuna na kusambaza kuanzia mwezi Machi hadi Oktoba
Sisi Kama Taifa ni Muda sasa wa kuacha mambo yasiyo ya Msingi na kujikita
na Fulsa kubwa kama hii,Tumeona MatokeoChanyA+ katika Korosho na Sasa Taifa
Turudi kujikita na kilimo na hasa kunapojitokeza fulsa mazao kama Parachichi,
kwa sasa wanaonufaika zaidi na Soko hili Ni wageni walioshtukia mapema Fulsa
hii.
No comments:
Post a Comment