Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
Watanzania
waliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Kikanda na Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustino Mahiga huku
ikiwakilishwa na Balozi wao nchini, Wang Ke. Kumbukumbu hiyo,
imeandaliwa na Jumuia ya Marafiki wa Tanzania na China ambayo Mwenyekiti
wake Dk.Salim Salim na Katibu wake ni Joseph Kahama.
Kabla
ya kuweka mashada kwenye makaburi kwenye makaburi ya wachina hao ambao
wengi wao ni wataalamu na wahandisi katika ujenzi wa reli, ilitolewa
historia fupi ya vifo vyao.
Akizungumza
baada ya kuweka mashada, Balozi Mahiga alisema ujenzi wa reli hiyo
ulithibitisha urafiki wa kutoka moyoni kati ya nchi hizo mbili na
kufafanua ujenzi wake ulifungua milango kwa China kujenga viwanda
vingine kama UFI na Kiwanda cha Nguo cha Urafiki.
"Wakati
wa ujenzi huu damu zilimwagika, wachina wamepoteza maisha na wengine
wamebaki na ulemavu wa kudumu...hivyo urafiki wetu sisi na China ni wa
damu," amesema.
Naye,
Balozi Wang amesema nusu ya karne iliyopita, kupitia ombi la Rais wa
Tanzania, Julius Nyerere na Rais wa Zambia, Kenneth Kaunda, viongozi wa
kizazi cha China, Mwenyekiti Mao Zedong na Waziri Mkuu, Zhou Enlai
walifanya maamuzi ya kimkakati na kihistoria kusaidia ujenzi wa TAZARA.
"Wafanyakazi
na mafundi Wachina 50,000 waliitikia wito wa taifa na waliungwa mkono
na wenzao kutoka Tanzania na Zambia, walishinda vigumu na vikwazo
vingine kumalizia ujenzi wa TAZARA yenye urefu wa kilomita 1,860 ndani
ya miaka sita na kuufanya kuwa mradi wa kihistoria wenye umaarufu
duniani,"alisema.
Amesema wafanyakazi na mafundi 65 Wakichina walipoteza maisha na walizikwa katika ardhi ya Afrika mbali na nyumbani kwao.
"TAZARA
imekuwa ikifahamika kwa dunia kama reli ya ukombozi iliyowasaidia watu
wa Afrika kupata Uhuru na Ukombozi...na pia reli ya urafiki ikiwakilisha
urafiki wa ndani kati ya Wachina na Waafrika,"amesema.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere,
Joseph Butiku amesema ipo haja kwa Tanzania na China kuendelea kudumisha
urafiki wao.
"Wakati
ule Mwalimu Nyerere kabla ya kwenda kuomba China watujengee reli
alianza kuomba kwa nchi moja ya Magharibi sihitaji, anaetaka kuijua aje
nitamnong'oneza. Nchi hiyo ilimjibu Nyerere hivi; ujenzi wa reli ya
Tanzania na Zambia upitie Zanzibar. Nyerere akaondoka tukaenda China na
baada ya kufika huko Mwalimu ikabidi aongee na waziri mkuu wa nchi hiyo,
Zhou Enlai.
"Tena
wakati anaomba hakwenda moja kwa moja alizunguka lakini hakujibiwa
chochote ila wakati tunataka kuondoka tulienda kuaga kwa Rais wa China
ambaye alikubali ombi letu. Kwa hiyo huu ni urafiki wa damu,"amesema.
Mnara
wa Makaburi ya Wachina waliokuwa wakijenga Reli ya Tazara ambao
walifariki wakati wa ujenzi wa reli hiyo miaka zaidi ya 40 iliyopita.
Waziri
wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi
Agustine Mahiga akitoa heshima na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang
Ke, kwenye Mnara wa makaburi ya Wachina waliofkuja kutengeneza Reli ya
Tazara
Waziri
wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi
Agustine Mahiga akiwa na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke,
wakiweka mashada kwenye moja ya kaburi la wakandarasi waliofika nchini
kujenga reli ya Tazara
Waziri
wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi
Agustine Mahiga akihutubia Viongozi na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
waliofikakatika sherehe ya kitamaduni ya watu wa china ya kuwakumbuka
mafundi waliojenga reli ya Tazara.
Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, akihutubia na kutoa historia
fupi ya ushirikiano wa Tanzania na China ulivyoasisiwa na Mwalimu
Nyerere.
Waziri
wa Katiba na Sheria , Profesa Paramagamba Kabudi akiweka maua kwenye
kaburi la wataalamu wa kichina waliokuwa wanajenga reli ya Tazara.
Kibao kinacho elezea utambulisho wa Makaburi ya Wataalam wa Kichina Gongolamboto
Katibu
wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akieleza namana Mwalimuj
Nyerere alivyoweza kuomba reli kwa kiongozi wa China Mau Sentum
Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi
Agustine Mahiga na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, pamoja na
Viongozi wengine wakiwa wamesimama nyimbo za Taifa za mataifa yote
mawili zilivyokuwa zikiimbwa.
watu
waliofika katika Sherehe za utamaduni za kuwakumbuka Wataalamu na
Wakandarasi walikuwa wanjenga reli ya Tazara kutoka china wakitoa
heshima zao kwenye mnara wa kaburi hilo
Baadhi ya Wazee walioshiriki kujenga Reli ya Tazara kwa kushirikiana na Wachina miaka 40 iliyopita.
No comments:
Post a Comment