UZINDUZI WA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA
WAFANYABIASHARA WADOGO
27 Machi, 2018 - Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
imezindua rasmi utoaji wa vitambulisho vya
Wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta
isiyo rasmi ikiwa ni pamoja na Wamachinga.
Utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara
hao unatokana na marekebisho ya Sheria ya
Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 yaliyofanywa na
Kikao cha Bunge la Bajeti la Mwaka wa
Fedha 2017/2018 ambapo moja ya marekebisho
hayo ni kuwatambua na kuwapatia vitambulisho
maalum wafanyabiashara wadogo walio kwenye
sekta isiyo rasmi.
Zoezi hili linatekelezwa na Mamlaka ya Mapato
Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala wa Usajili,
Ufilisi na Udhamini (RITA) pamoja na Idara ya Uhamiaji.
TRA kwa kushirikiana na wadau husika hapo juu,
ilianza kutekeleza jukumu hilo kwa kuutambua Umoja wa
Wamachinga wa Kariakoo jijini Dar es Salaam na
kufanikiwa kuwapatia vitambulisho vya Taifa na
Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)
ambapo leo hii baadhi yao wamepatiwa vitambulisho
maalum vya wafanyabiashara wadogo kama ishara ya
uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho hivyo.
Baada ya mafanikio haya, zoezi la kutambua vikundi
mbalimbali vya wafanyabiashara wadogo na kuwapatia
kitambulisho cha Taifa na Namba ya Utambulisho wa
Mlipa kodi linaendelea kufanyika nchi nzima.
Aidha, Ili wafanyabiashara wadogo waweze kupata
vitambulisho hivyo maalum wanatakiwa:-
Kujiunga katika vikundi maalum vinavyotambuliwa
kisheria na Serikali,
Kuwa na Kitambulisho cha Taifa,
Kuwa na Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi ya
kikundi alichojiunga nacho na
Kuchangia shilingi 10,000/=.
Vitambulisho hivyo maalum kwa wafanyabiashara
wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi vitadumu na
kutumika kwa kipindi cha miaka mitatu (3)
na vitakuwa na maelezo ya
mfanyabiashara husika kama vile:-
Jina na picha ya mfanyabiashara,
Jina la eneo analofanyia biashara,
Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi na
Sahihi ya mfanyabiashara.
Imetolewa na:
Charles E. Kichere
KAMISHNA MKUU
|
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akimkabidhi
mmoja wa wafanyabiashara kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya
Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar
es Salaam Machi 27, 2018. Pamoja naye ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (mwenye miwani) na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. |
|
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) na Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakipata maelezo kutoka kwa Afisa wa
Kodi, Dina Kaka jinsi ya kuandaa risiti ya kitambulisho cha
Mfanyabiashara wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho. |
|
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akimkabidhi
Mfanyabiashara Mshamu Nakukwa kitambulisho wakati wa uzinduzi wa zoezi
la utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. |
|
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akimkabidhi
mmoja wa wafanyabiashara kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya
Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar
es Salaam Machi 27, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia
Mjema na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. |
|
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akizungumza na
baadhi ya wafanyabiashara wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji
vitambulisho na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) Dar es Salaam
Machi 27, 2018. Kulia (kwake) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema,
Kamshna wa Kodi za Ndani, elijah Mwandumbya na Naibu Kamishana wa Kodi
za ndani, Abdul Zuberi. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akimkabidhi
mmoja wa wafanyabiashara kitambulisho na Namba ya Utambulisho ya
Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho Dar
es Salaam Machi 27, 2018. Pamoja naye ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (mwenye miwani) na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. |
|
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akimkabidhi
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara (Machinga) Steven Lusinde kitambulisho na
Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) wakati wa uzinduzi wa zoezi la
utoaji vitambulisho Dar es Salaam Machi 27, 2018. Kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo.
(Imeandaliwa na ROBERT OKANDA BLOGS)
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na baadhi ya wafanyabiashara wakati uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho
na Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN) kwa wafanyabiashara
(Machinga) Dar es Salaam Machi 27, 2018. Kushoto (kwake) ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere na viongozi waandamizi wa Mamlaka hiyo. |
|
Sehemu ya wafanyabiashara (Machinga) wakishiriki katika uzinduzi huo. |
|
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere (kushoto) na Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Kodi
Msaidizi, Mordekai Kibona jinsi ya kuandaa kitambulisho cha
Mfanyabiashara wakati wa uzinduzi wa zoezi la utoaji vitambulisho.
|
|
Mwenyekiti
wa Wafanyabiashara (Machinga) Steven Lusinde akiongea kushukuru TRA na
Serikali kwa ujumla kwa kuwatambu na kuahidi kutoa ushirikiano kwa
serikali kwani imedhihirisha inawajali na kuthamini mchango wao kwa
maendeleo ya nchi. |
|
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
waandamizi wa Mamlaka hiyo, viongozi wa Machinga, Manispaa ya Ilala na
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). |
|
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
waandamizi wa Mamlaka hiyo, viongozi wa Machinga na Manispaa ya Ilala. |
No comments:
Post a Comment