|
Mheshimiwa
Balozi Rajabu Luhwavi, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji (katikati),
wengine kutoka kushoto ni ndugu Albert Philipo, Afisa wa Wizara kutoka
Idara ya Diaspora (kushoto) na ndugu Nelson Nkini, Mwenyekiti wa
Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Msumbiji akikaribishwa katika
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 yanayojulikana kwa jina la FACIM
yaliyofanyika tarehe 27 Agosti hadi 2 Septemba 2018 Maputo nchini
Msumbiji. Ushiriki wa wafanyabiashara kutoka Tanzania uliratibiwa na
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia
Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji kwa kushirikiana na Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
|
|
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Carlos Agostinho do Rosário
wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 ya FACIM
alipotembelea banda la Tanzania na kukaribishwa na Bi. Getrude
Ngweshemi, Kaimu Meneja - Masoko ya Ndani wa TanTrade na Bw. Albert
Philipo, Afisa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje ambapo
alipatiwa maelezo kuhusu bidhaa za viwandani pamoja na vivutio vya
utalii wa Tanzania. |
|
Balozi
Rajabu Luhwavi akipokea maelezo kutoka kwa Afiisa wa Wizara, Bw. Albert
Philipo kuhusu bidhaa za Tanzania zilizoletwa na wafanyabiashara
mbambali kutoka Tanzania wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya
54 ya FACIM Maputo, Msumbiji. Wengine katika picha hiyo ni
wafanyabiashara kutoka Kampuni mbalimbali nchini Tanzania.
|
Mheshimiwa
Balozi Luhwavi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wafanyabiashara kutoka Tanzania walioshiriki katika Maonesho ya Biashara
ya Kimataifa ya 54 ya FACIM mjini Maputo. |
|
Gavana
wa Nampula, Mheshimiwa Victor Borges akiwa na Mheshimiwa Balozi Rajabu
Luhwavi kushoto kwake wakikata utepe wakati wa kufungua Maonyesho ya
Biashara Nampula tarehe 20 Agosti 2018. Maonesho hayo yalihusisha
wafanyabiashara kutoka Tanzania na wenyeji wa Msumbiji.
|
Mheshimiwa
Balozi Rajabu Luhwavi akitoa maelezo mafupi wakati wa ufunguzi wa
Maonyesho ya Biashara Nampula yaliyohusisha wafanyabiashara kutoka
Tanzania. Kwa
upande wake Balozi Luhwavi, alieleza kuwa maonesho haya ni ya kimkakati
kwa ajili ya kukuza na kuimarisha umoja, mshikamano na mahusiano ya
kiuchumi yaliyojengwa na waasisi wetu hayati Mwalimu Julius Nyerere,
aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; hayati
Sheikh Abeid Amani Karume, aliyekuwa rais wa kwanza wa Zanzibar na
hayati Samora Moises Machel, aliyekuwa rais wa kwanza wa Jamhuri ya
Msumbiji. Maonesho haya yalifungua fursa za masoko kwa bidhaa za viwanda
vya Tanzania pamoja na kuendeleza juhudi za utekelezaji wa diplomasia
ya uchumi kwa vitendo na kukuza uchumi, hususan uchumi wa viwanda.
|
|
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kilele cha maonesho ya bidhaa
za Tanzania mjini Nampula akiwa pamoja na Balozi Rajabu Luhwavi na
Katibu Mkuu wa Jimbo la Nampula, Bi. Veronica Langa wakipata maelezo
kuhusu teknolojia ya kisasa ya ufugaji samaki kutoka kampuni ya Dokaman
ya nchini Tanzania. |
|
Kutoka
kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mheshimiwa Rajabu Luhwavi,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Ndugu Juma Ali Juma, Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara TanTrade,
Bi. Anna Bulondo wakipata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya
A- Z Textile Mills inayojishughulisha na utengenezaji nguo, vifaa vya
plastiki, mifuko ya kuhifadhia mazao na bidhaa nyingine. |
|
Balozi
wa Tanzania nchini Msumbiji, Mheshimiwa Rajabu Luhwavi akiwa pamoja na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi |
No comments:
Post a Comment