Kongamano la
Pili la Sekta ya Sanaa na Ubunifu ya
Afrika Mashariki kuhusu Uwekezaji (2nd
Mashariki Creative Economy Impact Investment Conference) lenye kauli mbiu ‘Haki Ubunifu ni mali, Nikopeshe’ llilokuwa
la siku mbili Oktoba 11-12, 2018 limemalizika huku wadau na Wabunifu mbalimbali kutoka
Tanzania na Nchi za Afrika Mashariki wakipata kujadili changamoto katika sekta
hiyo.
Awali
akifungua kongamano hilo Oktoba 11,2018 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Idara ya uwekezaji Bwana Aritiside Mbwasi
ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage amesema Sekta ya ubunifu ina umuhimu wake
hivyo wadau wanatakiwa kuwaangalia kwa jicho la pili katika kuwasaidia
wabunifu ili kuendeleza mitaji yao kwani ina umuhimu wake kwa sababu ndio
inaleta biashara, huduma, bidhaa na teknolojia mpya.
Amefafanua
kuwa, ni jinsi gani ubunifu unaongeza
ufanisi kwa namna ya kipekee na
ubunifu huo unavyofanya kazi na kuachana
na kazi za mazoea.
“Wabunifu
wetu wanamawazo mengi. Kwa mfano
watumiaji wa Electroniki Media (digital) labda anaandaa program ya watoto namna ya kusoma ‘online’ huo ni ubunifu. Sasa changamoto taasisi za kifedha wao wanaangalia zaidi namna ada yao inavyoweza kurudi, lakini
wazo au ubunifu huo aliofanya huyo msanii je Benki pengine wasiuone
..biashara
inaweza kulipa kwa hiyo ni moja ya changamoto wanayokutana nayo wabunifu wengi
nchini na kwingine kote hapa Duniani” ameeleza Aritiside Mbwasi.
Kwa hatua
hiyo amebainisha kuwa, sekta hiyo inaumuhimu wake na mijadala ya kongamano hilo
itakuja na hitimisho la kuwasaidia wabunifu namna ya kupata mitaji.
Aidha,
amesema moja ya pendekezo pengine ambalo wadau hao wanatakiwa kuangalia ni
namna ya kushirikiana na wawekezaji
wengine ambao tayari wao wana fedha
ama mtaji ili kuingia ubia wa kuungana kwenye shea.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Maendeleo ya
Afrika Mashariki la (Culture and Development East Africa - CDEA), Bi Ayeta Anne Wangusa amesema kongamano hilo
lililoandaliwa kwa kushirikiano na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na
kuwezeshwa kwa msaada wa wadau wa OSIEA
na British Council, wanategemea wadau
washiriki watakuja na majibu juu ya wabunifu kupata mikopo kutoka kwa wadau
wenye mitaji.
Naye Mtaalmu
na mtafiti wa kimaitafa wa viwanda vya
ubunifu, Dkt. Keith Nurse, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Shirika la Dunia la Uchumi, kwenye tasisi ya Sir Arthur Lewis Institute for
Social and Economic Studies ndani ya chuo kikuu cha West Indies, amesema kuwa
wabunifu wengi Duniani wamekuwa na matamanio ya maendeleo makubwa lichaya
kukosa fursa tarajiwa kwa wakati.
Aidha, Dkt.
Nurse ametoa mifano jinisi haki ubunifu imetumika kama dhamana ya kukopesha
wabunifu kutoka nchi zilizoendelea na nchi
zinazoendelea.
Kongamano
limeendesha mijadala mbalimbali kutoka kwa
watalum wa sheria, fedha, haki miliki na haki ubunifu, kutoka Afrika
Mashariki.
Aidha, wadau
mbalimbali wanaoshughulikia masuala ya haki miliki kutoka serekalini na mashirika kama CISAC, wajumbe kutoka Jumuiya
ya Afrika Mashariki, Wizara zinahohusika na haki miliki toka nchi za jumuiya ya
Afrika mashariki,
Benki ya
Maendeleo Afrika Mashariki, Benki za
kiuchuni, wawekezaji wa Afrika mashariki, mawakili wa haki miliki, vyombo vya
hakimiliki vya Afrika Mashariki na wasanii mbalimbali kutoka Afrika Mashariki
wameudhuria kongamano hilo.
Mwisho.