Ikionesha ramani ya majengo mara baada ya kukamilika
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina kushoto,
akikabidhi mkataba kwa mmoja kati ya Mafundi Saba walioshinda zabuni ya
kujenga Hospitali.
Na Ofisa Habari Mufindi
Halmashauri
ya Wilaya ya Mufindi imetiliana saini na Mafundi Uashi saba (07),
watakaotekeleza kandarasi za awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali ya
kisasa ya Wilaya katika kata ya Igowole, eneo ambalo liliteuliwa rasmi
kuwa makao makuu mapya ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Hafla
fupi ya kusaini kandarasi hizo imefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi
Mtendaji, ambapo, jumla ya Majengo saba muhimu yatajengwa ambayo ni
Jengo la Utawala, Jengo la Wagonjwa wa nje, Jengo la kuhifadhia dawa,
Jengo la kufulia, Jengo la Mionzi, Jengo la Wazazi sanjari na Jengo la
Maabara ambayo yanatajikiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi nane
(08)
Aidha,
kiasi cha Fedha kitakachotumika kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi huu
mkubwa na muhimu kwa ustawi wa Afya za wakazi wa Mufindi ni shilingi
Milioni elfumoja na miatano (1,500) sawa na shilingi Bilioni 01 na
Milioni 500 zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Akizungumza
katika hafla ya kutiliana saini, Mwenyekiti wa Halmashari Mhe. Festo
Mgina, amewataka Mafundi hao kutekeleza maradi kwa wakati sanjari na
kuzingatia viwango vilivyokubalika na atahakikisha wanapata vifaa na
malipo yao kwa wakati ili Hospitali hiyo ikamilike kwa wakati na kuanza
kutoa huduma kwa wakazi wa Halmashauri ya Mufindi.
Naye
kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bw. Isaya Mbenje, ametoa rai kwa
wataalamu hao wa ujenzi kufanya kazi kwa weledi mkubwa, kuacha
visingizio vya mara kwa mara vitakavyochelewesha kukamilika kwa mradi.
“Pigeni
kazi Fedha tunayo, yote ipo kwenye akaunti inawasubiri ninyi, hivyo
yeyote atakayekwamisha tutavunja mkataba, atafukuzwa pamoja na
kufunguliwa mashitaka” akihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu huyo.
Imetolewa na
Ofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano
HALMSHAURI YA WILAYA MUFINDI
No comments:
Post a Comment