Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi
akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kupunguza madhara ya maafa
nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya
asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara iliyofanyika katika
Ukumbi wa Mazengo Dodoma hoteli Januari 28, 2019.
Mkuu
wa Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa kwa
Kanda ya Afrika, Amjad Abbashar akizungumza kuhusu namna bora za
kukabili majanga wakati wa warsha hiyo.
Mwakilishi
Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw.Alvaro
Rodriques akiwasilisha hotuba yake wakati wa warsha hiyo.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi
akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini
Tanzania,Alvaro Rodriques wakati wawarsha ya kupunguza madhara ya maafa
nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya
asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara iliyofanyika katika
Ukumbi wa mikutano Dodoma hoteli Januari 28, 2019.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi
pamoja na wajumbe wa meza kuu wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati
wa warsha hiyo.
Sehemu
ya wajumbe wakifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya Mwakilishi Mkazi wa
Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bwana Alvaro Rodriques
(hayupo pichani) wakati wa warsha hiyo.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi (wa
tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe
walioshiriki katika warsha hiyo.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi
akizungumza jambo na Mkuu wa Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa
ya Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Afrika, Amjad Abbashar (wa kwanza
kushoto) na katikati ni Mratibu wa Maafa wa Idara ya Maafa Bw.Charles
Msangi.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi
akiteta jambo na Watendaji wa Ofisi yake, katikati ni Kanali Matamwe
Said, Mkurugenzi, Idara ya Uratibu wa Maafa na kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara hiyo anayeshughulikia Mipango na Utafiti Bw.Bashiru
Taratibu
Serikali
kwa ushirikiana na wadau wengine imejipanga kuendelea kukabiliana na
majanga yanayoikumba nchi ili kuhakikisha inashughulikia na kutatua
majanga hayo pindi yanapotokea.
Hayo
yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge na
Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi Januari 28, 2019 wakati akifungua warsha
ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na
jamii dhidi ya majanga ya asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la
Sahara.
Tarishi
alibainisha jitihada zinazofanywa na Serikali ili kukabili maafa ikiwa
ni pamoja na kuendelea kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kuimarisha
ustahimilivu wa majanga ya asili kwa kuongeza idadi ya wilaya zenye
mipango ya kupunguza madhara ya maafa, kuboresha mifumo ya tahadhari za
awali, kuongeza utoaji wa elimu kwa umma na kuimarisha shughuli za
kujiandaa, kukabili na kuimarisha mfumo wa uratibu wa masuala ya maafa.
“Kwa
kuzingatia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka wa Mitano, 2016/17-
2020/21 tutaendelea kuimarisha ustahimilivu wa majanga ya asili pamoja
na kukabili majanga kwa kuzingatia utekelezaji wa malengo ya msingi ya
Mfumo wa Sendai wa Kupunguza Madhara ya Maafa wa mwaka 2015 – 2030,
tumedhamiria kuhakikisha tunakabiliana na majanga ili kujiletea
maendeleo,”alisema Tarishi
Aliongezea
kuwa, kwa kuzingatia majanga yanayoikabili nchi ikiwemo mafuriko nchi
haina budi kuwa mikakati hiyo ili kuhakikisha inakabili na kuweka
mikakati yenye tija katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini.
Tarishi
alibainisha kuwa, mafuriko yamekuwa na athari nyingi kwa kulinganisha
na majanga mengine yanayoikabili nchi mara kwa mara kwa kuzingatia
takwimu zilizopo kwa sasa.
“Takwimu
zinaonesha kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, 2018 mafuriko
yameathiri wilaya 50 na kusababisha vifo kwa watu 71, majeruhi kwa watu
64, kuharibiwa nyumba 15,802 kwa viwango tofauti, kuathiri miundombinu
katika shule 43, mashamba ya mazao mbalimbali, na vituo vya
afya,”alisisitiza Tarishi
Alieleza
kuwa, takwimu zilizopo tangu tupate uhuru nchi imeathiriwa na ukame
zaidi ya mara 18 ikimo yale ya mwaka 2006/2007 na 2007/2008 ambayo
yaliathiri zaidi mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Manyara,
Shinyanga, Lindi, Singida, Tabora na Mwanza.
Sambamba
na hilo Ukame mwingine mkubwa ulitokea mwaka 2008/2009 ulioathiri zaidi
mikoa ya kaskazini ya nchi hasa Arusha na Manyara. Mikoa ambayo mara
nyingi huathiriwa na ukame ni Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga,
ambayo kawaida hupata mvua ya chini kwa kiwango cha kati ya milimita 200
- 600 kwa mwaka.
Naye
Mkuu wa Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa
kwa Kanda ya Afrika, Amjad Abbashar, alieleza mipango mikakati ya
kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuzingatia ongezeko la
madhara yatokanayo ya maafa ikiwemo vifo, upotevu wa makazi, pamoja na
uharibifu wa mali za watu.
“Tutaendelea
kushirikiana na kuhakikisha tunakabili na kuzuia maafa yasitokee pale
itakapotokea ili kuendelea kuwa na maendeleo endelevu katika mazingira
tuliyonayo,”alieleza Abbashar
Kwa
upande wake Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini
Tanzania,Alvaro Rodriques, aliwataka wajumbe kuitumia fursa ya warsha
hiyo kwa kuzingatia mada zitakazowasilishwa ili kuhakikisha nchi
inaendelea kuwa na wataalam na mikakati yenye kutatua madhara yatokanayo
na majanga na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na
Serikali ya Tanzania katika kushughulikia maafa.
AWALI
Warsha
ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na
jamii dhidi ya majanga ya asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la
Sahara imeratibiwa na Idara ya Usimamizi wa shughuli za Maafa Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya
Maafa ya Umoja wa Mataifa na Taasisi ya Utafiti ya CIMA kupitia ufadhili
wa Umoja wa Ulaya. Aidha warsha inatarajiwa kudumu kwa siku tano hadi
Februari 01, 2019 Jijini Dodoma. Warsha hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa
programu ya Umoja wa Ulaya (EU) katika nchi za Africa, Caribbean na
Pacific (ACP), ambayo inalenga kupunguza majanga katika nchi hizo.
No comments:
Post a Comment