Waziri
wa Madini, Doto Biteko leo Januari 28, amekutana na Mzee Eric Mchata na
Kampuni ya madini ya Uranium ya Mantra Tanzania kwa lengo la kutatua
mgogoro uliopo baina ya pande hizo mbili.
Kikao
hicho, kinafuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Januari 22 na Mzee Mchata
wakati wa mkutano wa Kisekta ulioshirikisha wachimbaji wadogo na wadau
wa madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Wakati
akisikiliza kero za wachimbaji na wadau wa madini walioshiriki kikao
hicho, Rais Magufuli alipokea kero ya Mzee Mchata aliyemweleza kwamba
amekuwa na mgogoro na kampuni hiyo kwa kipindi cha takribani miaka 12 na
bado hajapata suluhu. Akijbu kero iliyowasilishwa na Mzee Mchata, Rais
Magufuli aliitaka Wizara ya Madini kuhakikisha mgogoro huo unafikia
mwisho.
Waziri
wa Madini Doto Biteko akimweleza jambo Mzee Eric Mchata wakati wa kikao
cha kusuluhisha mgogoro baina yake na kampuni ya Mantra Tanzania.
Waziri
wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mzee Eric Mchata. Kulia aliyekaa ni
Meneja Maendeleo, Utawala na RasilimaliWatu wa kampuni ya Mantra
Tanzania, Phillemon Tano.
Sehemu
ya Wataalam wa wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini wakifuatilia kikao
cha kusuluhisha mgogoro kati ya kampuni ya Mantra na Mzee Eric Mchata.
Kutoka kulia ni Kamishna wa Tume ya Madini, Prof. Abdulkarim Mruma,
Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Afisa Sheria wa Wizara ya
Madini, Joseph Nyamsenda.
No comments:
Post a Comment