Jopo
la Mawaziri Nane wametembelea bwawa la Mindu mkoani Morogoro kuangalia
namna bora ya sheria ya Usimamizi wa Sh rasilimali za maji kwa wananchi
waliondani ya mita 60 hadi 500 katika Bwawa hilo. Mawaziri Nane hao
walifika katika bwawa la maji la Mindu ambalo ndio linalisha maji kwa
asilimia 80 katika Manispaa ya Morogoro ambapo kwa sheria hiyo inataka
wakazi walioko katika mita zilizo ainishwa kuondoka kwa ajili ya
kuepusha madhara kwa wananchi pamoja na kulinda vyanzo vya maji.
Jopo
hilo limetokana na kauli ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kuunda Jopo
maalum kwa ajili kuangalia maeneo ambayo yanaingiliana na matatizo ya
ardhi na wananchi juu namna bora ya kutoleta madhara kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Jopo la Mawaziri ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Willam Lukuvi amesema kuwa Mamlaka ya Mkoa yahakikishe
inasitisha ujenzi wa makazi katika maeneo ya bwawa la Mindu pamoja
kuandika barua kwa waziri mwenye dhamana ya maji ili kutoa kibali cha
utekelezaji wa sheria kwa wananchi hao.
Lukuvi amesema utekelezaji wa sheria ya kuwaondoa wananchi isitishwe mpaka waziri atoe kibali.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe amesema wananchi
wanatengeneza utaratibu wa kutafuta maeneo ya kuwahamishia katika mpango
wa upimaji wa viwanja 3000 na kununua kwa fedha ndogo. Nae Afisa wa
Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani amesema sheria inakataza
wananchi kuingia au kufanya shughuli yeyote katika chanzo cha maji.
Ngonyani
amesema kuwepo kwa wananchi katika bwawa la Mindu kumeadhiri kupungua
kina cha Bwawa na kuongeza fedha katika kutibu maji kwa mamlaka ya maji
safi ya mkoa huo. Aidha amesema kuwa wanataka kuongeza kingo zaidi
katika bwawa hilo huku wafadhili wakitaka kuwaondoa wakazi katika maeneo
ya Mindu na Kasanga. Mhandisi Ngonyani amesema kuwepo kwa wananchi hao
kuna madhara makubwa ikitokea bwawa hilo kupasuka ambapo hivi karibuni
baadhi ya nchi kumetokea kupasuka kwa mabwawa na kuleta madhara makubwa.
"Kuwepo
kwa wananchi katika chanzo cha maji ni athari kubwa hivyo maisha ya
wananchi na usalama wa afya zao"amesema Ngonyani. Amesema kusitisha
baadhi ya shughuli za kibidamu katika bwawa la Mindu kumefanya kupungua
kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindu. Jopo la Mawaziri hao watapita katika
maeneo yenye changamoto katika Mikoa Morogoro, Mbeya, Kigoma, Mara,
Geita pamoja na Mwanza na kuja na suluhisho bora ya wananchi katika
kuondoa migogoro. Mawaziri hao katika Wizara Ofisi ya Rais-Tamisemi,
Kilimo, Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano -
Mazingira,Maliasili na Utalii,Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Ma kazi,Maji
pamoja na Mifugo na Uvuvi.
Naibu
Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akizungumza uwepo wananchi katika Bwawa
la Mindu na madhara ya kuwepo hapo katika Bwawa la Mindu.
Afisa
wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza
kuhusiana na sheria ya Usimamizi wa Rasilimali Maji ya wananchi kuvamia
katika eneo la Bwawa la Mindu.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe akizungumza katika bwawa la
Mindu wakati jopo la Mawaziri lilipotembelea Bawawa hilo.
Mwenyekiti
wa Jopo la Mawaziri , Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
William Lukuvi akizungumza na waandishi habari mkoani Morogoro mara
baada ya kutembelea Bwawa la Mindu lenye changamoto za kisheria.
Muonekano wa bwawa la Mindu mkoani Morogoro ambalo limevamiwa na wananchi
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii Morogoro
No comments:
Post a Comment