Na. Saja Kigumbe
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema serikali za Tanzania na
Misri zimekubaliana kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha nyama na mazao ya
ngozi hapa nchini.
Waziri
Mpina amebainisha hayo jana Februari 5,2019 ofisini kwake jijini
Dodoma mara baada ya kupata ugeni kutoka nchini Misri ukiongozwa na
Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit.
“Tunaenda
kujenga kiwanda kikubwa cha kusindika nyama, cha kusindika ngozi, cha
kusindika mazao ya ngozi, kiwanda ambacho hakipo katika nchi hizi zote
za Afrika ya Mashariki na Kati.” Alisema Mhe. Mpina
Waziri
Mpina amemuhakikishia waziri huyo wa Misri kuwa rasilimali za mifugo na
uvuvi zilizopo nchini zipo salama na kwamba wizara imekuwa ikifanya
jitahada kuhakikisha samaki hawavuliwi kwa njia haramu na hakuna
biashara haramu ili kuhakikisha rasilimali hizo zinanufaisha viwanda vya
ndani na wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta hizo.
Aidha
Waziri Mpina amemuarifu Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin
Aboussteit kuwa hakuna mifugo inayoruhusiwa kuingia nchini kutoka nje ya
nchi bila ya kuwa na vibali na kuwa usimamizi wa nchi katika rasilimali
za mifugo na uvuvi uko salama.
Katika
kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga
Mpina, kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Abdallah Ulega, makatibu wakuu wa wizara hiyo pamoja na manejimenti ya
wizara.
Waziri
wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit (kulia) akifafanua jambo
katika kikao hicho huku akisiskilizwa kwa makini na Naibu Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallaha Ulega na wajumbe wengine hawapo pichani
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (wa tatu kushoto) akizungumza
ofisini kwake baada ya kutembelewa na ujumbe kutoka Misri ukiongozwa na
Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit
No comments:
Post a Comment