Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame
Mbarawa, amefungua Mkutano wa Saba wa Mawaziri wa Maji wa nchi nane zilinazohusiana na Bonde la Mto Zambezi
(Zambezi Watercourse Commission – ZAMCOM) na kuitaka jamii ya mataifa hayo
kuona umuhimu wa kamisheni ya chombo hicho kuendelea kuimarika na kusimamia
raslimali za ZAMCOM kwa manufaa yaliyokusudiwa.
Waziri
Mbarawa alikuwa anafungua kikao cha Baraza la Mawaziri wa Maji katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere,
jijini Dar es Salaam, vikao vikiwa ni Mkutano wa Sita wa Baraza la Mawaziri
Februari 26 – 27 na Mkutano wa saba wa Kamati ya Wataalaam ya ZAMCOM, nchi
husika zikiwa ni Angola, Botswana, Msumbiji, Malawi, Namibia, Zambia, Zimbambwe
na Mwenyeji Tanzania.
Mkataba
wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi ulianza rasmi mwaka 2011 kwa lengo la
kusimamia raslimali za maji za Bonde la Mto Zambezi, Tanzania ambayo ni mwanachama
maji yake toka Ziwa Nyasa, kwa wastani wa asilimai 16 ya maji yaingiayo Ziwa
Zambezi kwa mito, humwagika Ziwa Zambezi
na Bonde hilo linahitaji hifadhi na zipo fursa za kuwepo miradi ya manufaa kwa
nchi hizo.
Baraza
limepokea Mpango kazi (Strategic Plan) na
Mfumo wa kubadilishana, kutumia
na kuhifadhi takwimu za raslimali za Maji kwa njia ya TEHAMA, ambapo Tanzania
imemaliza muda wake wa Uenyekiti na nafasi hiyo kupewa Zambia.
No comments:
Post a Comment