Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano
wa sita wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi nane la watumiaji wa
maji wa mto Zambezi utakao fanyika mnamo Februari 28 mwaka huu jijini
Dar Es Salaam.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji Profesa
Makame Mbarara wakati akiongea katika kikao cha waandishi wa habari
kilichofanyika mkoani Tanga hapo jana.
Alisema kuwa
Tanzania ni mmoja wa wanachama washiriki wa usimamizi wa maji katika
mabonde saba kati ya mabonde tisa yaliyopo katika ukanda wa mto
Zambezi.Hivyo alisema kuwa mkutano huo utatanguliwa na
mkutano wa saba wa wataalamu wa maji ambao utafanyika mnamo februari
26 na 27 mwaka huu jijini Dar Es salaama.
Alisema kuwa
mkutano huo unalenga katika kuweka mikakati ya namna ya kusimamia
raslimali za maji pamoja na kutunza mazingira ya vyanzo vya maji kwa
maendeleo endelevu ya nchi wanachama wa umoja huo.
“Takwimu zinaonyesha Tanzania kupitia bonde la ziwa Nyasa inachangia
karibu asilimia 11.3% ya maji yote yaliyoko katika Mto Zambezi huku
nchi nyingine zikichangia kwa kiwango kilichobaki”alisema Waziri
Mbarawa.
Pia alisema kuwa katika mkutano huo Mawaziri hao
wataweza kupata fursa ya kujadili na kupitisha mpango mkakati wa
matumizi ya maji ya mto Zambezi ukihusisha miradi mbalimbali ya sekta
hiyo.
“Tutaweza kujadili kwa pamoja taarifa ya hali ya
mazingira ya bonge hilo pamoja na kupitisha mwongozo wa namna ya
kubadilishana takwimu za raslimali za maji”alisema Waziri huyo.
Mawaziri wa nchi za Angola ,Botiswana,Zambia ,Zimbabwe,Botswana
,Msumbiji,Malawi,Namibia,na mwenyeji Tanzania wanatarajiwa kushiriki
katika mkutano huo
No comments:
Post a Comment