Vijana wa Kanisa la Living Water Center Kawe chini ya Apostle Onesmo Ndegi na Apostle Lilian Ndegi lililopo katika Manispaa ya Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wameshiriki katika zoezi la kuchangia damu
katika kilele cha wiki ya vijana kanisani
hapo.
Vijana hao waliamua
kushiriki katika zoezi hilo mapema siku ya Jumapili ikiwa ni katika kuunga mkono juhudi mpango wa Taifa wa Damu Salama chini ya Wizara ya Afya
wa kutoa damu ili kuokoa uhai wa wahitaji wa damu katika hospitali
nchini.
Akiongoza zoezi la uchangiaji damu Mchungaji wa Vijana Kanisani hapo
Albert Monyo aliwataka vijana katika jamii kuwa na moyo wa kutoa damu
ili kuwasaidia wenye uhitaji maana kwa kufanya hivyo kunasaidia
kupunguza uhitaji mkubwa wa damu uliopo kwenye hospitali nyingi hapa
nchini.
Naye Afisa muhamasishaji Damu Salama kanda ya Mashariki Mariam Juma
alitoa rai kwa waamini wa madhehebu mbalimbali na wanajamii kwa ujumla
kujenga tabia ya kuwa wanachangia damu mara kwa mara bila kusubiri
dharula.
Alisema uhitaji wa damu bado ni mkubwa na Ofisi
ya Damu Salama bado hijawahi kuziba pengo la upatikanaji wa damu ya
kutosha kwa asilimia mia moja.
Baadhi ya Vijana wachangiaji damu
wakimsikiliza Afisa Mshauri kutoka Damu Salama katika majadiliano kabla ya
kutoa damu.
Albert Monyo Mchungaji wa Vijana kanisani hapo akimsikiliza Afisa Mshauri kutoka Damu Salama katika majadiliano kabla ya kutoa damu.
Albert Monyo Mchungaji wa Vijana Kanisani hapo alipowaongoza vijana katika zoezi la uchangiaji damu
Afisa mshauri kutoka damu salama akimshauri mmoja wa wachangiaji damu katika zoezi hilo |
Mmoja wa wachangiaji wa damu akioesha kadi yake ya wachangiaji mara kwa mara |
Mmoja wa wachangiaji wa damu akioesha kadi yake ya wachangiaji mara kwa mara |
Maafisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama walioendesha zoezi hilo. |
Maafisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama walioendesha zoezi hilo |
No comments:
Post a Comment