Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo
amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Wanawake (UN-Women) Hodan Addou
aliyeambatana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez,
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na mambo mengine Mwakilishi huyo wa UN-Women alizungumzia kazi
mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo hapa nchini hususani katika
kushirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ikiwemo Mkakati wa
Kukuza Uchumi na kupumguza Umasikini Tanzania(MKUKUTA) na Mkakati wa
Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia)
akisalimia na Hodan Addou, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN-Women), mwingine pichani ni
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez ofisini kwa Makamu
wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia)
akizungumza na Hodan Addou, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN-Women), pamoja na Mwakilishi
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez (katikati) ofisini kwa
Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Hodan Addou, Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake
(UN-Women),pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro
Rodriguez (kushoto) ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es
Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia)
akitwa kwenye picha ya pamoja na Hodan Addou, Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN-Women), mara
baada ya kumaliza mazungumzo leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu
jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia)
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa
Alvaro Rodriguez mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa
Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment