Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh
Anthony Mavunde amewataka wanawake wa Dodoma Mjini kuchangamkia fursa
za kiuchumi na kutokubali kukatishwa tamaa kushiriki kwenye shughuli za
kiuchumi ili kujijengea heshima kubwa katika jamii.
Mavunde ameyasema hayo asubuhi
katika kongamano lilioandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania(CWT)
kitengo cha Wanawake katika Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya kilele cha siku ya MWANAMKE DUNIANI.
“Natamani kuwaona wanawake wa
Dodoma mkiwa mbele kuchangamkia fursa za kiuchumi ili kujijengea nguvu
ya kiuchumi na kujiongezea kipato.Dodoma hivi sasa baada ya tamko la
Makao Makuu fursa nyingi sana zimejitokeza hivyo msilaze damu kwa kubaki
kuwa waangaliaji na badala yake na ninyi mshiriki moja kwa moja”Alisema
Mavunde
Akisoma Risala kwa niaba ya walimu
hao kitengo “KE” Mwl Joyce Kaishozi ameeleza kwamba Chama hicho
kimejipanga vyema kumjengea uwezo mwalimu mwanamke ili jamii kutambua
nafasi ya Mwalimu Mwanamke na ndio maana katika kongamano walimu
wamepata nafasi kupata mafunzo katika maeneo ya AFYA,UJASIRIAMALI na
UONGOZI BORA.
Kongamano hilo pia lilihudhuriwa
na Mjumbe Wa Kamati Kuu CCM na Mlezi wa Mkoa wa Dodoma Ndg Leila Burhan
Ngozi na Mbunge wa Viti Maalum-Dodoma Mh Felister Bura
No comments:
Post a Comment