Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe Joketi Mwegelo akizungumza katika maadhimisho ya
Siku Kutenda Mema iliyofanyika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe, Joketi Mwegelo amesema kuwa ukuta kwa vijana ni
kutenda matendo yaliyo mema ikiwemo kusaidia au kutoa msaada pale penye
uhitaji, wakati wa Maadhimisho ya Siku Kutenda Mema 'Good Deeds Day'
iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es Salaam.
Amesema
hata vitabu vya Mungu vinafundisha kutenda mema ikiwemo kutoa pale
panapohitajika na mafanikio yake yataonekana kwa kile ambacho mtu
anajitoa. Mwegelo amesema hata yeye katika harakati zake vijana wenzake
wamekuwa na mchango mkubwa wa kujitoa bila kuangalia maslahi ya kifedha.
Aidha
amesema kuwa maadhimidlsho ya siku ya kutenda mema iwe ni njia ya jamii
kuangalia vitu vya kufanya katika kusaidia watu wengine.
Naye
Mwenyekiti wa Vipco na Mratibu wa Maadhimisho hayo, Emmanuel Makundi
amesema kuwa wameandaa maadhimisho kwa kutambua matendo mema ndio nguzo
ya amani, na matendo mema ni pamoja kuhakikisha kila mmoja anaishi kwa
amani.
Makundi amesema wamefanya mambo mbalimbali ya jamii na watu wamekuwa na mwitikio katika kuwaunga mkono wa kusaidia watu wengine.
Afisa
Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Mkoa wa Dar es Salaam,
Mariam Juma amesema kuwa mahitaji ya damu kwa nchi ni chupa laki tano
lakini ukusanyaji umefikia laki tatu hivyo wanahitaji wananchi
wajitokeze katika kuchangia damu.
Mwenyekiti
wa VIPCO Emmanuel Makundi akizungumza kuhusiana na maadhimisho ya siku
ya kutenda mema na mchango wa wadau mbalimbali yaliyofanyika katika
viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Vijana
wakichangia Damu katika maadhimisho ya Siku Kutenda Matendo mema
yaliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Afisa
Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama Mkoa wa Dar es Salaam
Mariam Juma akizungumza hali ya uchangiaji wa damu katika maadhimisho ya
Siku ya Kutenda Mema iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco Jijini
Dar es Salaam.
Picha
ya pamoja wakitangaza amani katika maadhimisho ya siku ya kutenda
matendo Mema iliyofanyika katika viwanja vya Don Bosco jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment