Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, ameongoza ujumbe wa Tanzania
kwenye mikutano ya kipupwe(Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayofanyika mjini Washington DC,
Marekani.
Akizungumza
kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Mjini Washigton DC, Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa ujumbe wa Tanzania
unaojumuisha pia wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi-Zanzibar,
utasimamia maslahi ya pande zote mbili za Muungano.
Mikutano
hiyo inatoa fursa kwa Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka
katika nchi wanachama ambao pia mi Magavana wa Benki ya Dunia na IMF,
kujadili maendeleo na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika
utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo na ushirikiano.
Aidha
Mikutano hiyo hutoa fursa kwa nchi kushiriki kama mwanahisa kwenye
mikutano ya kiutawala (Board of Governors) ya Taasisi hizo mbili ambapo
maamuzi ya kiuendeshaji na kisera hufanyika
Tanzania
itapata fursa ya kushiriki kwenye Kamati Maalum za Benki ya Dunia na
IMF na baadhi ya mikutano hiyo ni Mkutano wa Mawaziri wa Fedha
inayoshughulikia sera na utulivu wa Sekta ya fedha (International
Monetary Committee and Finance Committee-IMFC
Dkt.
Mpango atashiriki katika majadiliano na viongozi wa juu wa Benki ya
Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF wanaoshughulikia masuala ya
Afrika kuhusu utekelezaji wa program za sera za kiuchumi, mikopo nafuu
na misaada ya kitaalam kwa Tanzania.
Mazungumzo
hayo yatajikita kwenye maeneo ya mwenendo wa uchumi wa dunia; miradi ya
maendeleo iliyopendekezwa na Benki ya Dunia kwa mwaka 2019/20, kujenga
uwezo wa rasilimali watu, mahitaji ya kujenga uchumi wa kidijitali na
maeneo mengine ambayo Benki ya Dunia inaweza kusaidia kupatikana mikopo
nafuu ya kugharamia miradi ya kipaumbele hasa reli na umeme.
Waziri
wa Fedha pia anatarajia kupata fursa ya kukutana na Taasisi na
mashirika mbalimbali ya kimataifa, washirika wa maendeleo na wawekezaji
wenye nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini.
Dkt.
Mpango pia ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na watanzania kwa ujumla
kwamba Tanzania inafanya vizuri kiuchumi na kijamii na kumpongeza
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi, kwa jitihada kubwa
anazozifanya kuitangaza nchi na kusukuma mbele agenda za nchi
Kwa
Upande wake, Balozi Wilson Masilingi, akiukaribisha ujumbe wa Tanzania
nchini Marekani, amebainisha kuwa yeye na timu yake wamejipanga
kuhakikisha ushiriki wa nchi katika mikutano hiyo unakuwa mzuri na wenye
manufaa na mafanikio kwa Taifa.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati) akiongoza
kikao cha maandalizi cha Ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya Kipupwe
ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, kwenye Ofisi za
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania
nchini Marekani, Balozi Wilson Masilingi na Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania Prof. Florens Luoga, kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Khamis Mussa Omar
na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akiteta
jambo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Wilson Masilingi
wakati wa kikao cha maandalizi cha Ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya
Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF,
kilichofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani,
Mjini Washington DC.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Wilson Masilingi, akizungumza jambo
wakati wa kikao cha maandalizi cha Ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano
ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF,
kilichofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani,
Mjini Washington DC.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, akiwa katika kikao cha
maandalizi cha Ujumbe wa Tanzania kwenye Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya
Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, kilichofanyika kwenye Ofisi
za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mjini Washington DC.
No comments:
Post a Comment