Maana ya Ushiriki na Ushirikishwaji wa Wananchi.
Ni kuhusika na kuhusishwa kwa wananchi katika upangaji na
utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo katika kijiji au mtaa.
Vilevile kushiriki katika kuibua miradi na vipaumbele mbalimbali vya maendeleo na kutambua matatizo na kuibua mikakati ya utekelezaji katika ngazi ya kijiji na mtaa. Fursa anazopata mwananchi zinaweza kuwa za kisiasa na kiutendaji. Kisiasa kushiriki katika maamuzi na kiutendaji kushiriki kutekeleza yale yote yaliyoamriwa na wananchi
wenyewe kwa kushirikiana na viongozi wao.
Swala la kushiriki na kushirikishwa katika vijiji na mitaa ni la lazima kwani fedha za umma zimeanza kwenda katika ngazi za vijiji na mitaa kwa mfano fedha za elimu ya msingi MMEM, fedha kwa ajili ya elimu ya sekondari yaani MMES na fedha kwa ajili ya maendeleo ya jamii yaani TASAF na miradi mingine ya afya, kilimo n.k.
No comments:
Post a Comment