Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu Wenye
Ulemavu Mhe. Stella Ikupa ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha
kitengo kinachoshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu ili kuendana na
mahitaji halisi nchini.
Ameyasema
hayo hii leo Aprili 09, 2019 alipokuwa akijibu hoja Bungeni Dodoma
ikiwa ni moja ya hoja iliyotolewa kuhusu uboreshwaji wa kitengo hicho
ili kuendelea kuongeza nguvu katika kushughulikia mahitaji ya kundi
hilo.
Naibu
Waziri alieleza kuwa Ofisi yake imejipanga kuhakikisha inaboresha
kitengo hicho kwa kuendelea kuwajengea uwezo watumishi na kuongeza
watumishi watakaohudumia makundi hayo.
“Serikali
imeoa ipo haja ya kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hiki
wanaosimamia na kuratibu masuala ya watu wenye ulemavu ili kuongeza
nguvu na kuboresha utendaji,”alisema Ikupa
Aliongezea
kuwa, umuhimu wa kuongeza watumishi utasaidia kuendana na mahitaji
halisi ya kundi hilo na kupunguza changamoto zilizopo kwa sasa.
Katika
kuendelea kuboresha utekelezaji wa masuala hayo Ofisi ya Waziri Mkuu
inaendelea kuandaa mazingira wezeshi ikiwemo kuanzishwa kwa Mfuko wa
Taifa kwa Watu Wenye Ulemavu utakaosaidia kushughulikia masuala ya
ruzuku za vyama vya watu wenye ulemavu, kuwezesha programu za elimu na
mafunzo, kuwezesha huduma za utengamavu kwa watu wenye ulemavu pamoja na
kutumika katika tafiti mbalimbali.
“Kwa
mwaka wa Fedha 2019/2020 jumla ya shilingi Milioni 103 zimetengwa kwa
ajili ya Mfuko huo ambazo zitakuwa ni mbegu kwa mfuko hivyo ni vyema
sasa kukawa na wadau wataochangia kutunisha mfuko huu,”alisisitiza Ikupa
Aidha,
Serikali imeendelea kutoa elimu kwa mamlaka mbalimbali kuhusu ujenzi wa
miundombinu rafiki inayoendana na makundi ya watu wenye mahitaji maalum
nchini ili kuondokana na changamoto za uwepo wa miundombinu isiyoendana
na mahitaji halisi kwa kundi hilo.
”Suala
la Miundombinu ni la kila mtu hivyo basi ni vyema tukahakikisha
kunakuwa na ujenzi unaozingatia uhitaji wa wenye ulemavu ili kuepuka
changamoto zinazoweza kujitokeza”, alisisitiza Ikupa
No comments:
Post a Comment