Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akijibu swali bungeni leo
tarehe 17 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la
Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akijibu swali bungeni leo
tarehe 17 Aprili 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la
Bajeti Jijini Dodoma.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wizara
ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
imeanzisha mazungumzo na nchi wanachama wa COMESA na nchi kama Misri na
Algeria kupitia balozi zake ili kuandaa Makubaliano Maalum (Bilateral
Agreement) yatakayoiwezesha Tanzania kupeleka tumbaku kwa kodi nafuu.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) ameyasema hayo bungeni
Jijini Dodoma leo tarehe 17 Aprili 2019 wakati akijibu swali la Mhe
Edwin Amandus Ngonyani Mbunge wa Namtumbo aliyetaka kufahamu Wizara ya
Kilimo inashirikianaje na Wizara nyingine zinazohusika na uwekezaji wa
mambo ya nje kutafuta soko la tumbaku nchini Misri badala ya kulazimika
kutumia nchi za Uganda na Kenya pekee.
Mazungumzo
hayo yamefikia hatua nzuri na matarajio ni kufungua milango ya soko
hilo na hivyo kuongeza kipato kwa wakulima na taifa kwa ujumla. Aidha,
Makubaliano hayo yakikamilika Tanzania inaweza pia kuuza chai nchini
Misri na Algeria kwa faida kuliko ilivyo hivi sasa au badala ya kuuza
chai kupitia mnada wa Mombasa nchini Kenya.
Mhe
Bashungwa alisema kuwa mwaka 2014/2015 uzalishaji wa tumbaku ya moshi
(Dark Fire Cured Tobacco – DFC) ulisimama mkoani Ruvuma kutokana na
kukosa soko.
Hata
hivyo, Jitihada za Serikali ikawezesha Kampuni ya Premium Active
Tanzania Limited (PATL) kuonesha nia ya kununua tumbaku hiyo ya DFC
ambayo nchini Tanzania huzalishwa katika Wilaya ya Namtumbo na Songea
Vijijini Mkoani Ruvuma.
Alisema
Kampuni hiyo ilieleza kuwa lipo soko kubwa la tumbaku aina ya DFC
nchini Misri na Algeria lakini tumbaku ya Tanzania inauzwa kwa bei ya
juu kutokana na kodi inayotozwa ikilinganishwa na aina hiyo ya tumbaku
kutoka nchi za Uganda na Kenya kwa kuwa nchi hizo (Uganda, Kenya,
Algeria na Misri) ni wanachama wa jumuiya ya COMESA na kwa hiyo kodi za
kuingiza tumbaku, chai na bidhaa nchini Algeria na Misri kutoka Uganda
na Kenya ni za chini.
Mhe
Bashungwa alisisitiza kuwa, ili Tanzania iuze tumbaku, chai na bidhaa
nyingine katika nchi za Algeria na Misri kwa faida, inatumia nchi zilizo
kwenye jumuiya hiyo kama Uganda na Kenya.
No comments:
Post a Comment