Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
TAKRIBANI
Sh bilioni 20.3 zimefikishwa kwenye mfumo wa malipo wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) baada ya kugawa vitambulisho vya wajasiliamali
vipatavyo 1,022,178.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Selemani Jafo alipokuwa akizungumza na wakuu wa mikoa
kabla ya kupitia tathimini ya ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa
wajasiriamali.
Jafo
alisema kuwa kwa wakuu wa mikoa kugawa vitambulisho hiyo 1,022,178,
wajasiriamali wameweza kuchangia Sh bilioni 20.44 ambapo Sh bilioni 20.3
ndizo zilizoingizwa kwenye mfumo wa TRA na takribani Sh milioni 135.6
bado ziko mikononi wa wakusanyaji.
“
Mpaka kufikia Aprili 30 mwaka huu kiasi cha Sh milioni 942.47 zilikuwa
bado haijaingia kwenye mfumo wa mapato wa TRA, lakini nashukuru ndani ya
siku mbili hizi tatu wakuu wa mikoa wameweza kuzifikisha kwenye mfumo
fedha nyingi zaidi, niwapongeze kwa hilo.’
Jafo
alisema endapo fedha zinazokusanywa kutokana na vitambulisho vya
wajasiriamali hazitaingia kwenye mfumo wa mapato wa TRA basi fedha hizo
zinakuwa mbichi na kuna hatari ya kuwapo upotevu au kutumika katika
matumizi yasiyopangwa.
“
Nitumie fursa hii kuwahimiza wakuu wa mikoa na watendaji ambayo
wamekusanya fedha za vitambulisho vya wajasiriamali na kutoziingiza
kwenye mfumo wa malipo wa TRA kufanya hivyo mara moja,” alisema
Aidha,
Jafo aliwataka wakuu wa mikoa katika kuhakikisha azima ya Rais John
Magufuli ya kutaka wafanyabiashara wadogo watambuliwe na kuwaondolewa
usumbufu wanapofanya biashara zao na kushiriki katika uchumi wa nchi kwa
kuwaelimisha faida ya kuwa na vitambulisho hiyo.
“
Rais John Magufuli kiu yake ni kuwalinda wafanyabiashara wadogo na
kuwaona kuwa na sehemu ya kukuza uchumi wa nchi, alitaka wafanyabiashara
wadogo waondokane na adhana zilizokuwa zikiwapata kupitia askari wa
majiji ambao walikuwa wakitaifisha bidhaa zao na wakati mwingine
kugawana jambo ambalo haikuwa ni haki,”
Kwa
awamu ya kwanza na ya pili, vitambulishi vipatavyo 1,850,000 ambavyo
vilikuwa na thamani ya Sh bilioni 37 vilitolewa na mpaka Aprili 30 mwaka
huu, vitambulisho 1,022,178 vyenye thamani ya Sh bilioni 20.44
vimetolewa kwa wafanyabiashara wadogo.
Aidha,
Jafo aliipongeza mikoa ambayo imefanya vizuri katika ugawaji wa
vitambulisho vya wajasiriamali na ambayo ni Dar es Salaam iliyogawa
vitambulisho kwa asilimia 95.2. Tabora kwa asilimia 94.58, Kilimanjaro
kwa asilimia 79.05, Pwani kwa asilimia 77.66 na Tanga kwa asilimia 72.
Mikoa
ambayo imefanya viabaya na asilimia zake kwenye mabano ni
Katavi(asilimia 5.96), Njombe (asilimia 11.14), Rukwa (asilimia 25.03),
Iringa(asilimia 30.74) na Lindi (asilimia 33.58).
“
Tunajua changamoto ya baadhi ya mikoa na ndio maana tuko hapa tufanye
tathimini ya ugawaji wa vitambulisho hivyo, lengo letu ni kuwa lengo la
Rais la kuwalinda wale wasio na sauti lifikiwe kwa wajasiriamali wadogo
kutambuliwa,” alisema.
Mkuu
wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwandri alisema utaratibu wa kutoa
vitambulisho hivyo ulikuwa mgumu hasa kutokana na wananchi kuwa na dhana
ya kuwa Serikali inatumia vitambulisho hivyo kuwalipisha kodi.
“
Ukweli ulikuwa ni kuwa kiasi cha Sh 20,000 ni cha kugharamia
uchapishaji wa vitambulisho, lakini wengi waliona kuwa ni njia ya
kuwalipisha kodi.
Mwandri
aliongeza: “ Tuliweza kufanikiwa kwa kiasi hicho kwa kuwashirikisha
viongozi wa kimila, dini na watendaji kuanzia ngazi ya kitongoji, na
tukaitisha mikutano ya adhara ya kutoa elimu, na baada ya hapo mwitiko
wa wananchi ukawa mkubwa.”
Waziri
wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Mb) akifungua kikao kazi cha
Wakuu wa Mikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhusu tathmini ya ugawaji
wa vitambulisho vya wajasiriamali kilichofanyika St. Gasper Jijini
Dodoma.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Kichele akizungumza wakati wa kikao
kazi cha Wakuu wa Mikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhusu tathmini ya
ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali kilichofanyika St. Gasper
Jijini Dodoma.
Wakuu
wa Mikoa ya Tanzania Bara wakifuatilia kikao kazi kilichoitishwa na
OR-TAMISEMI ambacho kimehusisha Mamlaka ya mapato Tanzania kufanya
tathmini ya ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali.
Baadhi
ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wakifuatilia majadiliano
wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Mikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania
kuhusu tathmini ya ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali
kilichofanyika St. Gasper Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment