Naibu meya manispaa ya Iringa kupitia chama chama mapinduzi (CCM),Joseph Ryata akiwa na mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company Atanas Kipeto wakiwa katika kiwanda hicho cha kuchakata mpunga kuwa mchele
Naibu meya manispaa ya Iringa kupitia chama chama mapinduzi (CCM),Joseph Ryata akiwa na mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company Atanas Kipeto akiwa na wadau wengine waliofika katika kiwanda hicho
Mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company Atanas Kipeto akiwa katika kiwanda hicho
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Kiwanda cha Ruaha milling
company kuchakata mpunga kilichopo mkoani iringa kimetajwa kuwa mkombozi kwa
wakulima wa zao la mpunga ambalo limekuwa likilimwa kwa wingi katika wilaya ya
Iringa na mkoa wa mbeya.
Akiwa ametembelea kiwanda hicho
naibu meya manispaa ya Iringa,Joseph Ryata alisema kuwa kiwanda hicho kimejengwa
kwa kiwango cha kimataifa ambacho kitasaidia kukuza kipato cha wakulima wa zao
hilo.
“Kwa kweli jamani niseme ukweli
kiwanda hiki ni moja ya viwanda bora sana hapa nchini ambavyo vinachakata
mpunga kuwa mchele ukiangalia uwekezaji wake utagundua kuwa Ruaha milling
company kinakuja kuwa mkombozi kwa wakulima wetu” alisema Ryata
Ryata aliwataka wakulima wa zao
la mpunga kulima kwa wingi zao hilo kwa kuwa kiwanda cha Ruaha milling company
kinahitaji kiwango kikubwa cha zao hilo ili kufanya kazi kwa uhakika hivyo
wakulima jukumu lenu ni kulima kwa wingi na kwa ubora unaotakiwa.
“Naombeni nitoe rai kwa
wakulima kulima kwa wingi zao hili kwa kuwa kiwanda hichi kinahitaji kuwa na
tani nyingi za zao hilo la mpunga ili kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi
kwa ufanisi unaotakiwa” alisema Ryata
Ryata alisema kuwa kiwanda
hicho kimekuwa mkombozi kwa kuwa kinaongeza thamani ya zao hilo na kuongeza
kipato kwa wakulima wa nyanda za juu
kusini kwa kuanzisha kuwa na vifungashio ambavyo vinatoka katika kiwanda hicho.
“Kiwanda hichi kinafanya kila
kitu na kinatenga chenyewe kulinga na ubora wa mchele wenyewe hivyo wakulima
mnatakiwa kuwa na amani huku mkilima kilimo hicho kwa ubora unaotakiwa” alisema
Ryata
Aidha Ryata alisema kuwa
serikali inatakiwa kuendelea kuwaunga mkono wawekezaji wazawa kwa kuwa ndio
wanafanya kazi ipasavyo kwa kutoa faida inayotakiwa kwa taifa.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kiwanda cha Ruaha milling company,Atanas Kipeto alisema kuwa
lengo la kujenga kiwanda hicho ni kuhakikisha anakuza thamani ya zao la mpunga
na kukuza maisha ya wakulima ambao wamekuwa wakinyonywa na madalali.
“Mimi nimejenga kiwanda hiki
kwa lengo tu la kuwapa thamini yao wakulima wa zao la mpunga ambao wamekuwa
wakilima kwa taabu lakini hawapati ile faida au matunda yanayotakiwa kwa
kununua bei nzuri ambayo inafaida kwa wakulima” alisema Kipeto
Kipeto aliongeza kuwa amekuwa
akinunua zao la mpunga kwa kilo tofauti na wafanyabiashara wengine wanaonunua
kwa gunia ambao kwa asilimia kubwa wamekuwa wakiwanyonya wakulima kwa kununua
kwa kujaza lumbesa.
“Kununua kwa zao kwa kilo ni
kuongeza thamani ya mazao kwa wakulima na ndio njia pekee ya kuacha kuwanyonya
wakulima ambao ndio mara nyingi wamekuwa ngazi ya wafanyabiashara kutajirika”
alisema kipeto
No comments:
Post a Comment