Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara
baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei
26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo
na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika mazungumzo na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril
Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika
Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais
wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimpa zawadi ya picha ya wanyama Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril
Ramaphosa baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika
Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais
wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimkabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili na Kingereza pamoja na Vitabu
vya Kiswahili Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa kwa ajili
ya kujifunza lugha hio ya Kiswahili leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja
baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza
lake la Mawaziri.
Rais
wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa akisikiliza maelezo
yaliokuwa yakitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi kuhusu vitabu hivyo vya Kiswahili
leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa
Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimpongeza Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada
ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei
26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo
na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril
Ramaphosa wakati akizungumza na wanahabari Pretoria nchini Afrika Kusini
leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa
Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril
Ramaphosa wakifurahia jambo katika mazungumzo yao Pretoria nchini Afrika
Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa
Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada
ya kumaliza mazungumzo yao leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya
kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la
Mawaziri. PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 26 Mei, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri
ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa, Ikulu Jijini Pretoria.
Katika
Mazungumzo hayo, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Rais Ramaphosa kwa
kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Afrika Kusini na amemhakikishia
kuwa Tanzania itadumisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na
kihistoria na nchi hiyo ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius
Kambarage Nyerere na Hayati Nelson Mandela kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na Chama cha ANC (African National Congress).
Mhe.
Rais Magufuli amemshukuru, Mhe. Rais Ramaphosa kwa kumkaribisha kufanya
nae mazungumzo siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano
wa Afrika Kusini na amebainisha kuwa anatarajia uhusiano wa Tanzania na
Afrika Kusini utaimarishwa zaidi katika masuala ya uchumi na kukuza
lugha ya Kiswahili.
Kwa
upande wake, Mhe. Rais Ramaphosa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa
kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake, na amemhakikishia kuwa Afrika
Kusini inatambua mchango mkubwa wa Tanzania katika ukombozi wa Taifa
hilo na kwamba katika kipindi chake cha uongozi wake atauendeleza na
kuuza zaidi uhusiano huo.
Mhe.
Rais Ramaphosa amesema kufuatia uamuzi wa Afrika Kusini kuanza
kufundisha lugha ya Kiswahili, nchi yake itachukua walimu wa Kiswahili
kutoka Tanzania ili watumike kufundisha somo hilo katika shule za msingi
na sekondari.
Aidha,
Mhe. Rais Ramaphosa ameahidi kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini
Tanzania kabla ya Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC) uliopangwa kufanyika mwezi Agosti 2019 nchini
Tanzania. Na pia atahudhuria mkutano huo.
Kabla
ya mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba
Kabudi amemkabidhi Mhe. Rais Ramaphosa zawadi ya vitabu vya kusoma na
kufundishia lugha ya Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
Mhe.
Rais Magufuli na Mhe. Rais Ramaphosa wamefanya mazungumzo hayo ikiwa ni
kabla Mhe. Rais Ramaphosa hajatangaza Baraza lake la Mawaziri.
Mhe.
Rais Magufuli kesho ataondoka nchini Afrika Kusini na kuelekea nchini
Namibia ambako atafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa
Namibia Mhe. Hage Geingob.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Pretoria
26 Mei, 2019
No comments:
Post a Comment