Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mbele ya Makaburi ya
Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre mara baada ya kuweka
shada la maua.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akielekea kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia
yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre mara baada ya kuwasili katika eneo
hilo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka pamoja na mwenyeji wake
Rais wa Namibia Hage Geingob mara baada ya kuweka shada la maua katika Makaburi
ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa
Namibia Hage Geingob mara baada ya kuweka shada la maua katika Makaburi ya
Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua kiwanda cha nyama cha
Meatco kilichopo jijini katikati mwa mji wa Windhoek Namibia. PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 28 Mei, 2019 ametembelea na kuweka shada la maua katika eneo la
mashujaa (Heros Acre) waliopigania ukombozi wa Namibia, lililopo nje
kidogo ya Jiji la Windhoek nchini humo.
Katika
eneo hilo wamezikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia ambao baadhi yao
walipata mafunzo katika kambi ya Kongwa nchini Tanzania, wengine
walikuwa maafisa wa Chama cha SWAPO ambao ofisi zao zilikuwa Jijini Dar
es Salaam na wengine ni viongozi wakuu walioendesha mapambano wakiwa
nchini Namibia.
Baadhi ya mashujaa waliozikwa katika eneo hilo ni Ndimo Hamaambo, Peter Nanyemba, Theo-Ben Gurirabo na Toiro ya Toire.
Mhe. Rais Magufuli ameongozana na mwenyeji wake Mhe. Rais Hage Geingob.
Baada
ya kutembelea eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli ametembelea kiwanda cha
nyama cha kampuni Meatco kilichopo Jijini Windhoek na kuelezwa na Kaimu
Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bw. Jannie Breytenbach kuwa kiwanda kina
uwezo wa kuchinja ng’ombe 630 kwa siku, kimeajiri wafanyakazi 650 na
kwamba kampuni hiyo ipo tayari kushirikiana na Tanzania kuanzisha
viwanda vya nyama.
Mhe.
Rais Magufuli amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa idadi kubwa ya
mifugo Barani Afrika na ameikaribisha kampuni ya Meatco kuja kuwekeza
nchini Tanzania.
Katika
ziara hiyo, Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Luhaga Mpina, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba
Kabudi.
Kabla
ya kuondoka nchini Namibia kwenda nchini Zimbabwe ambako anakwenda
kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Zimbabwe Mhe.
Emmerson Mnangagwa, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo
na Rais Mstaafu wa Pili wa Namibia Mhe. Hifikepunye Pohamba Jijini
Windhoek.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Windhoek
28 Mei, 2019
No comments:
Post a Comment