MAJENGO
ya Wizara Tatu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliojengwa katika
eneo la Gombani Kisiwani Pemba Wilaya ya Chakechake yaliofunguliwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali
Mohamed Shein.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Magengo
Matatu ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zilioko katika eneo
la Gombani Wilaya ya Chakechake Pemba, kulia Waziri wa Fedha na Mipango
Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein, akikata utepe kuashiria kufungua majengo ya Wizara Tatu za
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kushoto Waziri wa Fedha na Mipango
Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa na kulia Waziri wa Kazi
Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico na
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Khamis Juma Maalim, wakishiriki katika
ukataji wa utepe huo wakati hafla ya ufunguzi wa majengo hayo.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akimsikiliza Mshauri wa Ujenzi wa Majengo Matatu ya Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Ndg. Mbarouk Juma, wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi
wa Majengo hayo eneo la Gombani Pemba.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein, akiuliza mswali wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa majengo hayo
katika eneo la Gombani Pemba.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akimsikiliza Mjenzi wa Majengo ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Ndg. Khamish Ali Khamis, ( na kushoto Mshauri Elekezi wa Mradi
wa Ujenzi huo Ndg. Mbarouk Juma.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akimsikiliza Kaimu Afisa Mdhamini Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee
Wanawake na Watoto Pemba Ndg. Hakim Vuai Shein, kulia, wakati
akitembelea jingo la Wizara hiyo.(Picha na Ikulu)
WAZIRI
wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa,
akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea majengo hayo baada ya
kuyafungua rasmin leo kisiwani Pemba katika eneo la Gombani.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akimsikiliza Mjenzi wa Majengo hayo wakati alitembelea majengo
hayo baada ya kuyafungua rasmin.
No comments:
Post a Comment