RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,
akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji
Zanzibar, katika mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo
iliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, kushoto Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.
Abdulhamid Yahya Mzee na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji
Dkt. Sira Ubwa.
WAZIRI
wa Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Zanzibar Dkt. Sira Ubwa
akiwasilisha Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yake wakati wa mkutano
huo uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
KATIBU
Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Ndg. Mustafa Aboud
Jumbe akiwasilisha Vifungu vya Matumizi na Mapato ya Wizara yake wakati
wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai 2018 hadi
March 2019, katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
BAADHI
ya Maofisa wa Idara za Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji wakifuatilia
mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni
Zanzibar.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment