Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Kutokuwepo
kwa Sera ya Ugatuaji Madaraka iliyojengwa kwenye mfumo wa Sheria ni
moja ya changamoto iliyofanya Serikali kufanya mapitio ya sera hiyo.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Selemani Jafo(Mb) wakati wa kufungua kikoa kazi
kilichokutanisha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kutoka Mikoa
yote 26 kwa ajili ya kutoa maoni na mapendekezo kwenye Rasimu ya Sera
ya Taifa ya Ugatuaji Madaraka ya 2019.
Alisema
kuwa changamoto moja wapo ni kutokuwepo kwa sera ya ugatuaji
iliyojengwa kwenye mfumo wa kisheria inayoelekeza mipaka, majukumu na
utaratibu wa utekelezaji wake, jambo ambalo linafanya ionekane kama ni
hiari na utashi (Voluntary and Willingness).
Jafo
alisema changamoto nyingine ni kuwepo kwa mitazamo inayokinzana kati ya
watendaji na viongozi wa kisiasa katika ngazi ya vijiji, kata na
halmashauri katika kuweka vipaumbele na kutekeleza miradi ya maendeleo
Aliongeza
kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikitegemea fedha kwa kiasi
kikubwa kutoka Serikali kuu na kutolea mfano kwa mwaka 2018 zilitegemea
zaidi ya asilimia 88 ya mapato.
“
Wizara za Kisekta kuandaa sera na sheria na kupeleka halmashauri kwa
ajili ya utekelezaji bila kuambatanisha rasilimali fedha, vifaa na
watu.”
Waziri
Jafo alibainisha kuwa uelewa mdogo wa dhana ya Ugatuaji wa Madaraka (D
by D) kwa baadhi ya Wizara za Kisekta na hivyo Sera hii kuonekana kama
ni suala ya OR-TAMISEMI kwa kiasi kikubwa imechangia kufanya Sera hii
kutotekelezeka kwa kiwango kilichotegemewa.
Jafo
aliongeza: “Kwa ujumla hatujafikia kiwango cha mafanikio
kilichotarajiwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeaza na
ndio maana Serikali imeamua kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Ugatuaji
ili kupata suluhisho la changamoto zilizojitokea.
Aidha,
Jafo amewataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kuhakikisha
wanashiriki kikamilifu katika kutoa maoni na mapendekezo hayo ili
kuboresha rasimu hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi, wadau na taifa kwa
ujumla.
Aidha
Jafo alitumia fursa hiyo kuwahimiza wakuu wa mikoa na makatibu tawala
wa mikoa kuhakikisha wanasimamia kwa ukabilifu fedha na utekelezaji wa
miradi mbalimbali ikiwamo ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa hospitali
za wilata, ujenzi wa mabweni, madarasa, vyoo katika shule za msingi na
sekondari ambayo tayari fedha zake zimeshatolewa na serikali.
Naye
Mwenyekiti wa wakuu wa mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng.
Evarist Ndikilo aliahidi kushiriki mzuri wa wawakuu hao kwa kuwa wao
ndio wanaotoka kwa wananchi.
Pia
alimhakikishia Waziri Jafo kuwa watasimamia kwa umakini utekelezaji wa
miradi ya maendeleo na kuwa itakamilika katika muda uliopangwa na kwa
ubora unaotakiwa.
Naye
Mwakilishi wa UNICEF, Pius Chaya alisema agenda ya mapitio ya Sera ya
Taifa ya Ugatuaji Madaraka imekuja wakati muafaka, kwasababu Serikali
inatakiwa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma wanazostahili na
ambazo zinawafikia kwa wakati.
Aidha,
Chaya alisema wadau wa maendeo ambao pia wameshiriki katika machakto wa
mapitio ya sera hiyo wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya
awamu ya tano katika kuwaletea wananchi wake maendeleo
Sera
ya Ugatuaji wa Madaraka ni dhana ya Kupeleka Madaraka, Majukumu na
Rasilimali kutoka Serikali Kuu kwenda kwa Wananchi kupitia vyombo vya
kidemokrasia na Kisiasa ambavyo, wajumbe wake huchaguliwa na kuwajibika
kwa Wananchi na vimepewa Mamlaka ya kutoa Maamuzi na kusimamia
rasilimali (yaani vina uhuru, vinajitawala, na vina hadhi ya kisheria).
Sera
hii ilianza kutekelezwa mwaka 1998 kupitia mpango wa maboresho ya
Serikali za Mitaa ikiwa na lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki
shughuli za Maendeleo katika maeneo yao na kuongeza ufanisi katika
uendeshaji wa shughuli za Serikali.
Waziri
wa Nchi OR-TAMISEMI Selemani Jafo akifungua kikao cha Wakuu wa
Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa
ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa St.
Gasper Jijini Dodoma.
Katibu
Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga akitoa taarifa ya utangulizi
kwenye ufunguzi wa kikao cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa
cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya ugatuaji wa madaraka
kilichofanyika katika ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma.
Baadhi
wa Wakuu wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Seleman
Jafo wakati akifungua kikao cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa ya
Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa St.
Gasper Jijini Dodoma.
Baadhi
wa Makatibu Tawala wa Mikoa wakimsikiliza Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI
Seleman Jafo wakati akifungua kikao cha kupitia rasimu ya Sera ya Taifa
ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa
St. Gasper Jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani
Jafo (watatu kutoka kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na
Wakuu wa Mikoa mara baada ya kufungua Kikao cha kupitia Sera ya Taifa ya
Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa
St. Gasper Jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani
Jafo (watatu kutoka kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na
Makatibu Tawala mara baada ya kufungua Kikao cha kupitia Sera ya Taifa
ya Ugatuaji wa Madaraka kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa
St. Gasper Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment